Pata taarifa kuu

Mkutano wa ujenzi wa Ukraine: Brussels yatoamsaada wa euro bilioni 50

Mkutano wa pili wa Kimataifa wa Ujenzi Mpya wa Ukraine unafunguliwa London siku ya Jumatano Juni 21, 2023. Mwaka jana, ulifanyika Lugano, Uswisi, pamoja na maafisa wa serikali. Kikao hiki kitatumika kuhamasisha sekta binafsi. Brussels inapendekeza kifurushi cha msaada cha euro bilioni 50 kwa Ukraine.

Jengo lililoshambuliwa kwa makombora ya Urusi mjini Kyiv siku ya Alhamisi, Juni 1, 2023.
Jengo lililoshambuliwa kwa makombora ya Urusi mjini Kyiv siku ya Alhamisi, Juni 1, 2023. AP - Alex Babenko
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini London, Emeline Vin

Zaidi ya washiriki elfu moja wanatarajiwa London, kibinafsi au kuwakilish makundi mbalimbali. Wawakilishi wa baadhi ya serikali sitini, viongozi wa biashara, wawekezaji, ambao kwa siku mbili watatafakari juu ya mustakabali wa kiuchumi wa Ukraine, kujiandaa kwa kipindi cha baada ya vita.

London inaeleza kuwa huu si mkutano wa wafadhili, bali ni kuwafanya wadau katika kiuchumi kutaka kuwekeza tena nchini Ukraine. Serikali ya Uingereza, ambayo tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi imejiweka kama mmoja wa wafuasi wakuu wa Ukraine, itazindua jukwaa la "matchmaking" kwa wafanyabiashara, na pia ni kwa sababu ya kutangaza mfuko wa "nishati ya kijani" wa euro milioni 110.

Benki ya Dunia inakadiria gharama ya kujenga upya na kufufua Ukraine kwa zaidi ya dola bilioni 400 katika kipindi cha miaka kumi ijayo. Kiasi kinachotarajiwa kuongezeka kwa muda mrefu kama vita vinaendelea, na ambayo inafanya Kyiv kutegemea mshikamano wa kimataifa.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kuhutubia mkutano huo kwa njia ya video. Hotuba ya Waziri Mkuu wa Ukraine, ambaye anakosoa kabisa vikwazo vya Uingereza dhidi ya Urusi, pia imepangwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.