Pata taarifa kuu

Ukraine yaendelea kuripoti kupata mafanikio, Urusi ikizidisha mashambulio

NAIROBI – Wakati huu ikiwa ni zaidi ya wiki moja sasa tangu Ukraine ianzishe mashambulio dhidi ya wanajeshi wa Urusi, Kiev imeendelea kuripoti kupata mafanikio ambapo inadai imechukua vijiji zaidi ya 8, licha ya Moscow kuzidisha mashambulio mjini Kiev.

Ukraine imeripoti kupata mafanikio katika uwanja wa mapambano
Ukraine imeripoti kupata mafanikio katika uwanja wa mapambano AP - Evgeniy Maloletka
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na maafisa wa ngazi ya juu ni kuwa Jeshi la Ukraine limeanza kukabiliwa na upinzani kutoka kwa wanajeshi wa Urusi, licha ya kuwa bado hawajafikia kiwango cha juu cha kumdhibiti mvamizi.

Akihojiwa na vyombo vya habari katika êneo la mto Mokri Yaly afisa kutoka kikosi cha 68 cha Ukraine, Lermontov amesema ikiwa atafika katikati mwa Donetsk pamoja na kikosi anachoongoza hakika atasema kwamba misheni yao, imekamilika huku akionyesha umuhimu êneo hilo.

Taarifa ya jeshi la Ukraine imesema Vikosi vya Kyiv vinasonga mbele, na hata jeshi la Urusi linathibitisha kwamba nafasi zake huko Urozhaine, kilomita nyingine mbili (zaidi ya maili moja) kusini mwa Blagodatne, zimeshambuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.