Pata taarifa kuu

Marubani wa ndege za kijeshi wa Ukraine waanza kupewa mafunzo Poland

Poland imeanza kutoa mafunzo kwa marubani wa Ukraine kuhusu ndege aina ya F-16, kulingana na mkuu wa diplomasia ya Ulaya Josep Borrell.

Ndege ya kivita ya Marekani F-16 CJ ikirusha kombora la AGM-65D Maverick wakati wa Mazoezi ya mwaka 2002.
Ndege ya kivita ya Marekani F-16 CJ ikirusha kombora la AGM-65D Maverick wakati wa Mazoezi ya mwaka 2002. © commons.wikimedia.org
Matangazo ya kibiashara

Poland imeanza kutoa mafunzo kwa marubani wa Ukraine kwa ndege za kivita za Marekani F-16 na nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya ziko tayari kutoa ndege hizo kwa Ukraine, Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell ametangaza leo Jumanne.

"Nina furaha kwamba hatimaye mafunzo ya marubani wa ndege aina ya F-16 yameanza katika nchi kadhaa, nchini Poland kwa mfano. Itachukua muda, lakini mapema itakuwa bora", ametangaza mwanzoni mwa mkutano wa Mawaziri wa Ulinzi wa Umoja wa Ulaya, EU, huko Brussels kuhusu msaada wa kijeshi kwa Ukraine.

"Tumepata idhini kutoka Washington kwa mafunzo ya ndege aina ya F-16 na tunafanya kazi kwa ratiba madhubuti ya kuanza mafunzo. Ni muhimu kufanya hivi haraka iwezekanavyo", ameelezea Waziri wa Ulinzi wa Uholanzi, Kajsa Ollongren. "Kwanza, tunaanza na mafunzo. Usambazaji wa vifaa utakuwa hatua inayofuata," ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.