Pata taarifa kuu

Ziara ya Rais wa Poland nchini Ukraine: Poland yatangaza kuunga mkono Kyiv

Vifaru vizito vya kwanza vya Ulaya vitakavyotumwa nchini Ukraine bila shaka vitakuwa vya Poland, ikiwa Ujerumani, nchi ambayo inatengeneza vifaru maarufu Leopard, itathibitisha mpango huu. Tangazo lililotolewa Jumatano huko Lviv, magharibi mwa Ukraine, na Rais wa Poland Andrzej Duda, ambaye alikutana na mwenzake wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, akiambatana na Rais wa Lithuania, Gitanas Nauseda. 

Marais wa Ukraine na Poland Volodymyr Zelensky na Andrzej Duda wanakumbatiana, huko Lviv, Januari 11, 2023.
Marais wa Ukraine na Poland Volodymyr Zelensky na Andrzej Duda wanakumbatiana, huko Lviv, Januari 11, 2023. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Huko Ulaya, mipango inaongezeka kwa minajili kusambaza vifaru kwa jeshi la Ukraine, kwa hofu ya shambulio jipya la Urusi mwishoni mwa msimu wa baridi. Na serikali ya Poland iko katika harakati ya kuagiza vifaru hivi, kauli ambayo ilipelekea Rais Andrzej Duda, apokelewa kwa shangwe vifijo katika mitaa ya mji wa Lviv.

Kabla ya kurudi Poland Jumatano jioni, Andrzej Duda alisimama kwa dakika chache katika Soko la Lviv Square… Haraka sana, mkuu wa nchi ya Poland alizungukwa na umati wa Waukraine ambao waliimba wakitaja jina lake, uku wakimshika mkono, kumbusu, na kumshukuru  kwa lugha ya Poland.

Andrzej Duda alitangaza jana, Jumatano, kwamba nchi yake itapeleka kwa Ukraine karibu kambi nzima ya vifaru aina ya Leopard-2, yaani vifaru vizito zaidi ya kumi na mbilivilivyotengenezwa na Ujerumani, akisisitiza juu ya hitaji la muungano wa kimataifa kuipa Ukraine vifaru hivyo kwa haraka iwezekanavyo  inavyohitaji kuzuia mashambulizi ya Urusi ...

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.