Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE MAPIGANO

Mamluki wa Wagner washirki katika mapigano nchini Ukraine

Wanajeshi wa Urusi, wameendeleza mashambulio Mashariki mwa Ukraine, hasa katika mji wa Soledar, na kusababisha vikosi vya Kiev kurudi nyuma, huku kundi la mamluki wa Wagner pia likishiriki kwenye mapigano hayo, likiwa kwenye mstari wa mbele.

 Mji wa Soledar nchini Ukraine
Mji wa Soledar nchini Ukraine REUTERS - CLODAGH KILCOYNE
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amekiri kuwa mji wa Soledar, umeharibiwa kutokana na mashambulio ya wanajeshi wa Urusi, lakini mji jirani wa Bakhmut, bado upo mikononi mwa vikosi vya nchi yake.

Uingereza nayo kupitia ripoti zake za kiusalama, inasema, wanajeshi wa Urusi na wapiganaji wa Wagner kwa sasa wanadhibiti mji huo na wanapigana katika mstari wa mbele, unaofahamika katika uzalishaji wa chumvi, katika jimbo hilo la Donbas, baada ya kuongeza mashambulio katika kipindi cha siku nne zilizopita.

Wachambuzi wa vita vinavyoendelea wanasema, jeshi la Urusi kudhibiti mji wa Soledar ni hatua kubwa sana kwao, wakati huu wanapoendeleza mapambano ya kuuchukua mji wa Bakhmut.

Hata hivyo, Uingereza inasema haitakuwa rahisi kwa Urusi kuchukua mji wa Bakhmut kwa sasa kwa sababu ya uthabiti wa vikosi ya Ukraine, lakini makabiliano makali ya kijeshi yanatarajiwa katika siku zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.