Pata taarifa kuu

Urusi: Jenerali Valeri Guerassimov aongoza operesheni nchini Ukraine

Urusi imembadilisha tena Jumatano hii, Januari 11 kamanda wa "operesheni yake maalum" nchini Ukraine, kwa kumteua Jenerali Valeri Guerassimov, ambaye hadi sasa amekuwa Mkuu wa Majeshi. Tangazo kutoka wizara ya Ulinzi linabaini kwamba Sergueï Surovikin anakuwa naibu na hivyo kutoa nafasi kwa mkuu wa majeshi.

Jenerali Valery Guerassimov, upande wa kushoto, akiwa na Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu, kwenye Ikulu ya Kremlin, mjini Moscow, Desemba 2022.
Jenerali Valery Guerassimov, upande wa kushoto, akiwa na Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu, kwenye Ikulu ya Kremlin, mjini Moscow, Desemba 2022. AP - Alexey Maishev
Matangazo ya kibiashara

Kamwe kamanda wa operesheni hakuwahi kuchukua muda mrefu kwa majukumu yake nchini Urusi. Sergueï Surovikin hata hivyo atakuwa ametekeleza majukumu yake kwa muda wa miezi mitatu pekee.

Uteuzi wake ulipongezwa na muungano wa Kadyrov-Prigojine, dhidi ya majenerali wa jeshi, ambao utendaji wao ulishtumiwa na viongozi hao wawili, lakini pia wanablogu wa kijeshi, kwa maneno makali.

Sergei Surovikin ambaye aliteuliwa siku ya mashambulizi ya angani dhidi ya daraja la Kerch, Oktoba 8, ndiye aliyeagiza wanajeshi wa Urusi kuondoka katika jimbo Kherson, aliongoza kampeni ya mashambulizi makali dhidi ya miundombinu ya nishati ya Ukraine, alizindua ujenzi wa ngome na mitaro katika maeneo yaliyotekwa na Urusi.

Ni vigumu kujua kama atakaye chukuwa mikoba yake atatangaza awamu mpya katika mzozo huo, kama vile mashambulizi ya Urusi kutokana na hali mbaya katika uwanja wa vita. 

Hayo yanajiri wakati mapigano makali yanaendelea kati ya vikosi vya Urusi na Ukraine leo Jumatano katika mji wa Soledar, mashariki mwa Ukraine, uliokuwa na idadi ya watu wapatao 10,000 kabla ya vita hivyo.

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema leo kuwa jeshi lake la anga limeuzingira mji wa Soledar na kukata njia za mawasiliano kutoka upande wa kaskazini na kusini. Msemaji wa wizara hiyo ya ulinzi Igor Konashenkov amesema, "Katika muendelezo wa mashambulizi kuelekea eneo la Donetsk, vikosi vya Urusi vimeyakomboa makaazi ya Pidhorodne katika jamhuri ya watu wa Donetsk. Jeshi letu la anga limekata njia za mawasiliano za upande wa kaskazini na kusini mwa mji huo. Jeshi limefanya mashambulizi dhidi ya ngome za adui."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.