Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE- MAPIGANO

Mapigano yanaedelea katika mji wa Soledar Ukraine

Ukraine inasema, wanajeshi wake wameendelea kupambana kuudhibiti tena mji wa Soledar katika jimbo la Donetsk, lakini inapata upinzani mkali kutoka kwa wanajeshi wa Urusi.

Makabiliano katika mji wa Soledar,Ukraine
Makabiliano katika mji wa Soledar,Ukraine AFP - ANATOLII STEPANOV
Matangazo ya kibiashara

Naibu Waziri wa Wizara ya Ulinzi, Ganna Malyar, amesema mapigano makali yanaendelea na licha ya upinzani mkali, vikosi vya nchi yake vinapambana ili kusonga mbele.

Wiki hii kundi la wapiganaji la Wagner, lilidai kuwa kwa ushirikiano na wanajeshi wa Urusi, vikosi vyake vilikuwa vimedhibiti mji huo wa Soledar lakini Ukraine inakanusha.

Naye msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov amewasifu wanajeshi wa nchi yake kwa kuuteka mji huo, wakati huu akimtangaza Jenerali Valery Gerasimov kuongoza vita nchini Ukraine.

Urusi imeongeza mashambulio wiki hii kwa lengo la kudhibiti kijeshi jimbo lote la Donestsk ambalo mwaka uliopiuta, iliandaa kura ya maoni na kuamua kuwa êneo hilo liko katika ardhi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.