Pata taarifa kuu

Yevgeny Prigojine ashutumu jeshi la Urusi kwa kushambulia kambi za Wagner

Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Urusi la Wagner ameshutumu jeshi la Urusi kwa kufanyamashambulizi ya anga kwenye kambi za wapiganaji wake nyuma ya uwanja wa vita dhidi ya Ukraine, na kusababisha "idadi kubwa ya waathiriwa".

Kulingana na kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Urusi la Wagner, Yevgeny Prigojine, jeshi la Urusi linarudi nyuma katika maeneo kadhaa ya kusini na mashariki mwa Ukraine.
Kulingana na kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Urusi la Wagner, Yevgeny Prigojine, jeshi la Urusi linarudi nyuma katika maeneo kadhaa ya kusini na mashariki mwa Ukraine. AP
Matangazo ya kibiashara

"Wamefanya mashambulizi ya makombora, kwenye kambi zetu. Idadi kubwa sana ya wapiganaji wetu wameuawa,” amesema Yevgeny Prigojine katika ujumbe wa sauti uliotangazwa na idara yake ya vyombo vya habari, akiahidi "kujibu" mashambulizi haya yaliyoagizwa na Waziri wa Ulinzi wa Urusi, kulingana na kiongozi huyu wa kundi la wanamgambo wa Urusi la Wagner. Hata hivyo jeshi la Urusi linakanusha kuwa limefanya mashambulizi ya anga kwenye kambi za kundi hilo.

Hayo yanajiri wakati Ukraine inadai kuangusha zaidi ya makombora kumi na mbili ya cruise ya Urusi usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa. Makombora haya yalilenga uwanja mdogo wa ndege wa kijeshi magharibi mwa nchi, kulingana na Jeshi la Wanahewa.

Kwingineko jeshi la Urusi linarudi nyuma katika maeneo kadhaa ya kusini na mashariki mwa Ukraine, anasema kiongozi wa kundi la wanamgambo la Wagner, akipingana na matamshi ya Kremlin kwamba mashambulio ya Kiev yalishindwa.

"Jeshi la [Urusi] linajiondoa katika maeneo ya Zaporizhia na Kherson, wanajeshi wa Ukraine wanasonga mbele," Yevgeny Prigozhin amesema katika mahojiano ya video yaliyotumwa kwenye Telegram na hidara yake ya vyombo vya habari.

"Hali kama hiyo inafanyika huko Bakhmout, adui atapenya zaidi na zaidi katika ulinzi wetu," mfanyabiashara huyo ameongeza, akimaanisha mji wa mashariki ambao Warusi wanadai kuwa wameuteka lakini Waukraine wanasema wamepiga hatua kwenye ukingo katika wiki za hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.