Pata taarifa kuu
MAPIGANO-USALAMA

Kyiv yashambulia daraja la kimkakati linalounganisha Crimea na Ukraine

Daraja moja linalounganisha eneo la Crimea na eneo la kusini mwa Ukraine linalokaliwa kwa sehemu na wanajeshi wa Urusi limeharibiwa na shambulio la Ukraine, mamlaka ya ndani ya Urusi imesema leo Alhamisi.

Наслідки обстрілу Чонгарського мосту
Наслідки обстрілу Чонгарського мосту © via REUTERS - VLADIMIR SALDO VIA TELEGRAM
Matangazo ya kibiashara

"Usiku, shambulio la anga limelenga daraja la Tchongar. Hakuna majeruhi yaliyoripotiwa,” amesema gavana wa Urusi wa Crimea Sergei Aksionov, akiongeza kuwa uharibifu huo unatathminiwa na kutoa wito kwa wakaazi watulie. Daraja hili linaunganisha Crimea iliyoshikiliwa na Moscow mnamo 2014 na eneo la jimbo la Ukraine la Kherson linalokaliwa na vikosi vya Urusi.

Shambulio lililoripotiwa na mamlaka ya Urusi linakuja wakati vikosi vya Ukraine vimekuwa vikifanya mashambulizi tangu mapema mwezi Juni katika maeneo kadhaa ya vita, hasa kusini mwa Ukraine. Crimea hutumika hasa kama ghala la vifaa kwa vikosi vya Urusi vilivyotumwa kusini mwa Ukraine.

Kama Sergei Aksionov alitaja daraja moja tu lililoathiriwa, afisa wa uvamizi wa Urusi huko Kherson ameripoti miundombinu kadhaa iliyoathiriwa, bila kutoa maelezo zaidi. Vikosi vya Kiev " vililipua miundombinu ya kiraia: madaraja kwenye mpaka wa kiutawala kati ya mkoa wa Kherson na Crimea karibu na Tchongar," amesema Vladimir Saldo, aliyeteuliwa na Moscow kama mkuu wa maeneo yanayoshikiliwa na Urusi huko Kherson. Amerusha hewani picha zinazoonyesha daraja moja na kreta kwenye njia kuu na kudai kwamba kulingana na "makadirio ya mapema" vikosi vya Kyiv vilitumia makombora ya Uingereza ya Storm Shadow.

Haikuwezekana kuthibitisha madai haya kwa uhuru. Crimea inalengwa mara kwa mara na mashambulizi ya Ukraine, hasa kutoka kwa ndege zisizo na rubani. Mnamo mwezi Oktoba 2022, mlipuko mkubwa uliharibu vibaya daraja pekee linalounganisha moja kwa moja Crimea na Urusi.

Likijulikana kama "Lango la Crimea", Daraja la Chongar ni mojawapo ya madaraja pekee yanayounganisha Crimea - iliyotwaliwa na Urusi mwaka 2014, ikitoa njia mbadala ya ukanda mwembamba wa ardhi unaounganisha Crimea na bara. Kwa upande wa Ukraine, kuharibu daraja hili kunaweza kuipa faida katika ufufuaji wa rasi hii na kuwa ngao katika mazungumzo yajayo.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.