Pata taarifa kuu

Urusi yaapa kupambana na uasi wa wapiganaji wa Wagner

Nairobi – Mkuu wa wapiganaji wa Wagner ameapa kupindua uongozi wa juu wa jeshi la Urusi. Moscow imemshutumu Yevgeny Prigozhin, kiongozi wa kundi la mamluki la Wagner, kwa kutishia vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Wapiganaji wa Wagner wameapa kuangusha uongozi wa jeshi la Urusi
Wapiganaji wa Wagner wameapa kuangusha uongozi wa jeshi la Urusi REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumamosi, Prigozhin alichapisha ujumbe wa sauti kwenye programu ya mtandao wa kijamii wa Telegram, akidai kuwa wapiganaji wake walikuwa wamevuka kutoka Ukraine hadi mji wa mpaka wa Urusi wa Rostov-on-Don - na kwamba wangepigana na mtu yeyote ambaye atajaribu kuwazuia.

Wapiganaji wa Wagner wamekuwa wakipigana na nchini Ukraine kwa niaba wa Urusi
Wapiganaji wa Wagner wamekuwa wakipigana na nchini Ukraine kwa niaba wa Urusi REUTERS - STRINGER

“Sote tuko tayari kufa. Wote 25,000, na wengine 25,000," alisema, baada ya awali kuwashutumu wakuu wa Urusi kwa kuanzisha mashambulio  dhidi ya watu wake."Tunakufa kwa ajili ya watu wa Urusi."

Wagner wanalishutumu jeshi la Urusi kwa kushambulia ngome zake
Wagner wanalishutumu jeshi la Urusi kwa kushambulia ngome zake REUTERS - STRINGER

Baadaye alichapisha video yake akiwa katika makao makuu ya kijeshi, ambayo yanasimamia mapigano nchini Ukraine, na kudai kuwa majeshi yake yamechukua udhibiti wa vituo vya kijeshi katika mji huo, ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege.

Video na picha zilizochapishwa mtandaoni, zikiwemo na shirika la habari la TASS la Urusi, zilionyesha watu wenye silaha wakizunguka majengo ya utawala huko Rostov na vifaru vilivyowekwa katikati mwa jiji. Haikufahamika watu hao wenye silaha walikuwa ni akina nani.

Wapiganaji wa Wagner wameonekana katika baadhi ya maeneo nchini Urusi
Wapiganaji wa Wagner wameonekana katika baadhi ya maeneo nchini Urusi REUTERS - STRINGER

Huduma za Usalama za Shirikisho zilisema hatua za Prigozhin ni "wito wa kuanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe kwenye eneo la Shirikisho la Urusi na kuchomwa mgongoni kwa wanajeshi wa Urusi wanaopigana na vikosi vya Ukraine vinavyounga mkono ufashisti."

Kujibu, viongozi wa Urusi walisema usalama umeimarishwa katika mikoa kadhaa na meya wa Moscow alitangaza kwamba hatua za "kupambana na ugaidi" zilikuwa zinachukuliwa katika mji mkuu.

Urusi kwa upande wake imeapa kupambana na wapiganaji wa Wagner
Urusi kwa upande wake imeapa kupambana na wapiganaji wa Wagner REUTERS - STRINGER

"Kwa lengo la kuzuia vitendo vya kigaidi vinavyowezekana katika eneo la mji wa Moscow na mkoa wa Moscow, operesheni ya kupambana na ugaidi imeanzishwa," kamati ya kitaifa ya kupambana na ugaidi ilinukuliwa na mashirika ya Kirusi ikisema.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema katika taarifa iliyowaandikia wapiganaji mamluki wa Wagner kwamba "wamedanganywa na kuingizwa kwenye tukio la uhalifu" na Prigozhin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.