Pata taarifa kuu
MAREKANI-USHIRIKIANO

Uganda: Marekani yamuwekea vikwazo mkuu wa idara ya ujasusi wa kijeshi

Mkuu wa idara ya ujasusi wa kijeshi nchini Uganda, Meja Jenerali Abel Kandiho, analengwa na vikwazo vya Marekani: Wizara ya Fedha ya Marekani ilitangaza Jumanne. Mali za afisa huyo mwandamizi nchini Marekani sasa zimezuiwa. Sababu eilizzotolewa ni kuhusika kwake katika kesi za ukiukaji wa haki za binadamu.

Maafisa wa ujasusi wa kijeshi, kulingana na wizara ya Fedha ya Marekani, wamewakamata, wamewaweka kizuizini na kuwashambulia raia.
Maafisa wa ujasusi wa kijeshi, kulingana na wizara ya Fedha ya Marekani, wamewakamata, wamewaweka kizuizini na kuwashambulia raia. AFP - CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Chini ya uongozi wa Meja Jenerali Abel Kandiho, maafisa wa ujasusi wa kijeshi, kwa mujibu wa wizara ya Fedh ya Marekani, wamewakamata, kuwaweka kizuizini na kuwashambulia raia "kwa sababu ya uraia wao, maoni ya kisiasa na ukosoaji wa serikali." "

Marekani inashutumu maafisa wa kijasusi wa Uganda kwa kuwaweka kizuizini watu hao bila kufuata utaratibu, na kuwafanyia ukatili ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kingono na shoti za umeme.

Mashtaka ambayo Flavia Byekwaso, msemaji wa jeshi la Uganda aliyatupilia mbali katika taarifa yake, akisema "amesikitishwa" na uamuzi uliochukuliwa na nchi mshirika bila "mashitaka ya haki". Amebaini kwamba ufafanuzi utaombwa kutoka kwa mamlaka ya Marekani.

Mashirika mengi ya kutetea haki za binadamu yalikashifu mamia ya visa vya ukiukwaji wa haki unaofanywa na idara ya ujasusi ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na kutoweka kwa watu waliomikononi mwa vyombo vya dola, wakati wa kipindi cha uchaguzi mwezi Januari mwaka huu.

Mwezi Aprili, waziri wa mambo ya ndani alikabidhi bungeni orodha ya zaidi ya watu 1,300 waliokamatwa na vyombo vya sheria kuhusiana na uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.