Pata taarifa kuu

DRC: EAC, Kenya zakanusha kujiuzulu kwa mkuu wa kikosi cha Jumuiya

NAIROBI – Jumuiya ya Afrika Mashariki, inasema barua inayosambaa ikieleza kuwa aliyekuwa Kamanda wa kikosi cha Jeshi cha Jumuiya hiyo kutoka nchini Kenya Meja Jenerali Jeff Nyaga, aliiandika na kujiuzulu ni uongo na inapaswa kupuuzwa. 

Meja Jenerali Jeff Nyagah
Meja Jenerali Jeff Nyagah © EACRF
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo la Jumuiya, limekuja baada ya Jeshi la Kenya, pia kutoa taarifa kama hiyo na kusema kuwa Kamanda huyo wa zamani hakujiuzulu kama inavyoelezwa. 

Katika barua hiyo, ilielezwa kuwa Kamanda huyo wa zamani wa kikosi hicho aliamua kuachana na majukumu yake kwa kuhofia usalama wake na kuwepo kwa kampeni chafu ya vyombo vya habari nchini DRC kuchafua operesheni ya kikosi hicho na hivyo kutatiza kazi zake. 

Alipozungumza na RFI Kiswahili kwa njia ya simu, Meja Jenerali Nyagah, alithibitisha kuondoka kwake nchini DRC na kusema alikuwa amerejea Nairobi kwa mashauriano, ambako ameteuliwa kwenye nafasi nyingine katika jeshi la Kenya. 

Hata hivyo, ripoti za ndani za kidiplomasia na  kutoka serikali ya DRC zimethibitisha uhalali wa barua hiyo. 

Kikosi cha Jeshi la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki,kinaundwa na mataifa saba baada ya kuundwa mwezi Aprili mwaka uliopita, kusaidia kuleta utulivu Mashariki mwa DRC na kupambana na makundi ya waasi, likiwemo lile la M23. 

Barua hii ilisambaa kwa sehemu kubwa siku ya Ijuma ya hapo jana haswa katika mitandao ya kijami nchini DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.