Pata taarifa kuu

DRC: Rekodi kuhusu ulinzi wa haki za binadamu inatiliwa shaka.

Nairobi – Rais Felix Tshisekedi, alipoingia madarakani baada ya uchaguzi wa mwaka 2018, aliahidi kumaliza siasa za uonevu zilizodumu kwa miongo kadhaa pamoja na kukabiliana na vitendo vya rushwa.

Alipoingia madarakani baada ya uchaguzi wa mwaka 2018, aliahidi kumaliza siasa za uonevu zilizodumu kwa miongo kadhaa pamoja na kukabiliana na vitendo vya rushwa
Alipoingia madarakani baada ya uchaguzi wa mwaka 2018, aliahidi kumaliza siasa za uonevu zilizodumu kwa miongo kadhaa pamoja na kukabiliana na vitendo vya rushwa AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo wakati huu akijiandaa kutetea nafasi yake katika uchaguzi wa Desemba 20 mwaka huu, rekodi kuhusu ulinzi wa haki za binadamu inatiliwa shaka.

Kwa majuma kadhaa sasa mashirika ya kutetea haki za binadamu ya ndani na nje ya nchi wakiwemo wapinzani wake, wameishutumu Serikali ya Tshisekedi kwa kuwabana wakosoaji wake kama ilivyokuwa kwa utawala uliopita.

Tayari nchi za Marekani na washirika wake wameonesha kuguswa na maandalizi finyu kuelekea uchaguzi
Tayari nchi za Marekani na washirika wake wameonesha kuguswa na maandalizi finyu kuelekea uchaguzi AFP - JACQUES WITT

Tuhuma hizi zinatokana na matukio ya hivi karibuni ikiwemo mauaji ya waandamanaji kwenye mji wa Goma, kutumiwa mambo ya machozi kuwatawanya wafuasi wa upinzani, kushikiliwa kwa wanahabari, wanasiasa na mauaji ya mwanasiasa Cherubin Okende.

Aliyekuwa waziri wa zamani Chérubin Okende
Aliyekuwa waziri wa zamani Chérubin Okende AP - Samy Ntumba Shambuyi

Kwa mujibu wa ripoti za mashirika kadhaa za kutetea haki za binadamu, uhuru wa vyombo vya habari na watu kutoa maoni, unajaribiwa, Alisema Jean-Claude Katende rais wa shirika la ASADHO.

Hata hivyo madai haya yamekanushwa vikali na msemaji wa Serikali Patrick Muyaya na yule wa rais Tshisekedi, Tina Salama.

Aidha tayari nchi za Marekani na washirika wake wameonesha kuguswa na maandalizi finyu kuelekea uchaguzi wa Desemba pamoja na matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.