Pata taarifa kuu
AFRIKA-CAF-SOKA-MICHEZO

Kombe la Mataifa bingwa barani Afrika

Barani Afrika, mwaka huu nchi ya Morroco ilijiondoa kuwa mwenyeji wa michuano ya soka kuwania taji la Mataifa bingwa barani Afrika kwa hofu ya ugonjwa hatari wa Ebola, uliozuka katika nchi za Afrika Magharibi, Liberia, Sie releon na Guinea.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka barani Afrika CAF, Issa Hayatou, akichukua uamzi wa kuipitisha Equatorial Guinea kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la mataifa barani Afrika.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka barani Afrika CAF, Issa Hayatou, akichukua uamzi wa kuipitisha Equatorial Guinea kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la mataifa barani Afrika. AFP PHOTO / STEPHANE DE SAKUTIN
Matangazo ya kibiashara

 

Shirikisho la soka barani Afrika lilikataa kuahirisha michuano hiyo, na kutafuta nchi nyingine itakayoaandaa michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Mwezi Novemba nchi ya Equitorial Guinea ilikubali kuandaa michuano hiyo itakayoanza tarehe 17 mwezi Januari hadi tarehe 8 mwezi Februari.

Novemba 3 mwaka 2014, Shirikisho la soka barani Afrika CAF lilitangaza kwamba michuano ya Kombe la mataifa barani Afrika itachezwa kama ilivyopangwa Januari 17 hadi Februari 8 mwaka 2015.

Hata hivyo shirikisho hilo liliipa muda Morocco ili iwe imekwisha chukua msimamo

hadi Novemba 8. Morocco iliomba michuano ya Kombe la mataifa barani Afrika iahirishwe ikihofia mambukizi ya virusi vya Ebola kwa wachezaji na watu watakao kuwa wamekuja kuhuzuria michuano hiyo.

CAF hatimaye iliamua rasmi kuachia michuano hiyo ichezwe katika muda uliyopangwa. Michuano hiyo itaanza kuchezwa Januari 17 hadi Februari 8.

Hata hivo Fifa iliunga mkono uamzi wa Shirikisho la Soka Afrika CAF ambao umezitaka mechi inayohusisha moja ya mataifa yanayo athirika kuchezwa katika nchi ambayo haijaathirika.

Oktoba 28 mwaka 2014, Fifa ilichapisha mapendekezo kuhusu namna ya kudhibiti Homa ya Ebola, huku ikibaini kwamba maandalizi kuhusu kombe la dunia la vilabu yanaendelea vizuri “ kama ilivyopangwa”.

Kwa sasa Equaterial Guinea ndio mwenyji wa michuano hiyo. Miongoni mwa viwanja vitakavyotumika ni pamoja na uwanja wa taifa wa mjini Bata wa Estadio de Bata wenye uwezo wa kuchukua mashabiki elfu 35 na mia 7, uwanja mwingine ni ule wa klabu ya The Panters wa mjini Malabo Nuevo Estadio de Malabo wenye uwezo wa kuchukua mashabiki elfu 15.

Uwanja mwingine ni ule wa klabu ya Atletico Malabo “Estadio Internacional wenye uwezo wa kuchukua mashabiki elfu 6, huku uwanja mwingine ukiwa ni ule wa Estadio La Paz wenye uwezo wa kuchukua mashabiki elfu 10.

Uwanja mwingine ambao unatarajiwa kutumika ni ule wa Estadio Manuel Enguru na uwanja wa Estadio La Libertad mjini Malabo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.