Pata taarifa kuu
KENYA-AL SHABAB-UGAIDI-USALAMA

Suala la ugaidi lawagawanya wabunge Kenya

Nchini Kenya, baadhi ya wabunge wanamshinikiza kiongozi wao bungeni Aden Duale kujiuzulu baada ya kusema kuwa kwa muda wa mwezi mmoja ujao atatoa orodha ya watu wanaoshirikiana na kundi la kigaidi la Al Shabab kutoka Somalia.

Wanajeshi wa Kenya wakiwasili katika Chuo kikuu cha garissa, kulikotokea shambulio la kigaidi lililogharimu maisha ya watu 148, ikiwa ni pamoja na wanafunzi 142. Γ  l'universitΓ© de Garissa, le 4 avril.
Wanajeshi wa Kenya wakiwasili katika Chuo kikuu cha garissa, kulikotokea shambulio la kigaidi lililogharimu maisha ya watu 148, ikiwa ni pamoja na wanafunzi 142. Γ  l'universitΓ© de Garissa, le 4 avril. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Wabunge hao wamesema, viongozi kutoka Kaskazini Mashariki mwa Kenya wanachukua muda mrefu kutoa majina hayo na kusisitiza kuwa Duale ajiuzulu wadhifa wake kabla ya kutoa majina hayo.

Hata hivyo, Duale amesema hatajiuzulu na kueleza kuwa wanasiasa kutoka Kaskazini mwa nchi hiyo wanafanya bidii kuhakikisha kuwa wanapigana na ugaidi.

Wakati huo huo mjadala unaendelea nchini Kenya ikiwa vijana waliojiunga na kundi la Al Shabab nchini Somalia waliopewa siku 10 wajisalimishe na kusamehewa ikiwa itakuwa ni sahihi kusamehewa.

Baadhi ya wabunge nchini humo wmeasema ikiwa watajisalimisha wachukuliwe hatua huku viongozi wa Kiislamu wakitaka serikali kuongeza muda huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.