Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Operesheni ya pamoja ya majeshi ya DRC na Uganda yanaendelea mashariki mwa DRC

Vikosi vya Uganda kwa ushirkiano na vile vya DRC vimeendelea na operesheni yao ya pamoja, dhidi ya waasi wa ADF kwa siku ya pili hapo jana, yenye lengo la kukomesha mashambulizi ya wapiganaji wa kijihadi wa ADF wanaotekeleza mauaji makubwa nchini Congo lakini pia nchini Uganda.  

Waasi wa ADF wamenyoonyesha kidole kwa mashambulizi kadhaa, hasa dhidi ya raia. Hapa, wanajeshi wa DRC wakikagua shambulio karibu na mji wa Oicha, karibu na Beni.
Waasi wa ADF wamenyoonyesha kidole kwa mashambulizi kadhaa, hasa dhidi ya raia. Hapa, wanajeshi wa DRC wakikagua shambulio karibu na mji wa Oicha, karibu na Beni. © Al-hadji Kudra Maliro, AP
Matangazo ya kibiashara

Operesheni za pamoja kati ya DRC na majeshi ya Uganda zinaendelea katika eneo la Beni, katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Mashambulizi ya anga na hatua za ardhini zinatekelezwa dhidi ya ngome za kundi la ADF, serikali na jeshi la DRC wamethibitisha tangu Jumanne.

Katika kusubiri hotuba ya rais wa DRC, Desemba 15, ambayo itagusia pia swala hilo la operesheni za pamoja, serikali na jeshi wametoa taarifa Jumanne hii kuhusu operesheni zinazoendelea.

Vikosi vya ardhini kutoka Uganda vimeingia kupitia kijiji cha Mobili ambapo duru kutoka katika maeneo hayo zinasema wananchi wamewapokea bila hofu yoyote. Wananchi wa maeneo hayo wamekuwa na ushirikiano na upande wa pili wa Uganda hasa ukizingatia kuwa wakulima wa Kahawa hupeleka kuuza nchini Uganda.

Jeshi la Congo linasema kila kitu kitakuwa wazi katika operesheni hiyo ambapo watafanya mkutano na vyombo vya habari, huku waandishi wa habari wa Beni nao pia watapata fursa ya kuhoji maswali. msemaji wa jeshi huko Beni amesema vikosi maalum vyenye uzowefu wa kupigana msituni tayari vimewasili na kwa muda wowote vitatumwa kwenye uwanja wa mapambano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.