Pata taarifa kuu
UGANDA-ULINZI

Uganda yadai kupata mafanikio makubwa katika operesheni yake dhidi ya waasi wa ADF DRC

Jeshi la Uganda linasema, linapata mafanikio makubwa baada ya kuanza mashambulizi ya anga dhidi ya waasi wa ADF, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Gari la jeshi la Uganda liliegeshwa chini ya mlima wa Rwenzori, karibu na mji wa Kichwamba (kusini-magharibi mwa Uganda), karibu na DRC.
Gari la jeshi la Uganda liliegeshwa chini ya mlima wa Rwenzori, karibu na mji wa Kichwamba (kusini-magharibi mwa Uganda), karibu na DRC. Gaël Grilhot/RFI
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Jeshi nchini humo Brigedia Flavia Byekwaso, amesema waasi wa ADF pia watasakwa na kikosi maalum, huku akitetea uamuzi wa jeshi kuvuka mpaka na kuingia DRC siku ya Jumanne, baada ya wabunge wa upinzani, kuhoji hatua hiyo.

Kwa upande wa FARDC, hakuna maelezo kuhusu operesheni hii. Luteni Antony Mwalushayi, msemaji wa Operesheni Sokola 1, amewataka tu wananchi kuwa na utulivu, akibainisha kuwa jeshi la Kongo linaendelea na operesheni katika eneo hilo.

Katika ujumbe wa Twitter uliochapishwa Jumanne, Novemba 30, msemaji wa serikali ya DRC, Patrick Muyaya, alitangaza kwamba "jeshi la DRC, FARDC, na jeshi la Uganda wameanza mashambulizi ya pamoja ya anga na kurusha mabomu kutoka upande wa Uganda dhidi ya ngome za magaidi wa ADF nchini DRC".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.