EAC: TotalEnergies kutathmini upya ununuzi wa ardhi kwa ujenzi wa bomba la mafuta
Nairobi – Kampuni ya mafuta ya Ufaransa TotalEnergies imetangaza mpango wa kutathmini upya ununuzi wa ardhi kwenye mradi wake wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Uganda kupitia nchini Tanzania, unaokosolewa na wanamazingira.
Imechapishwa:
Cheza - 00:58
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kampuni hiyo kubwa ya mafuta ya Ufaransa TotalEnergies imesema kwamba ujumbe wake umepewa jukumu maalum katika kuhakikisha mapitio ya kila hati iliyoafikiwa na pande zote inauwiana na utafiti uliofanywa hivi karibuni katika nyanja ya ardhi ya miradi yake ya mafuta nchini Uganda na Tanzania, Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) na Tilenga, ambayo inakabiliw ana upinzani mkubwa kutoka kwa wanaharakati wa mazingira kutoka Uganda.
Kampuni ya TotalEnergies inaendelea na mradi wake wa kuchimba visima vya Tilenga nchini Uganda na Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) lenye urefu wa kilomita elfu moja mia nne arobaini na tatu linalosafirisha mafuta hadi pwani ya Tanzania.
Taarifa ya Total Energies inasema kwamba Ujumbe wa maafisa wake utatathmini taratibu za utwaaji ardhi zilizotekelezwa, masharti ya mashauriano, fidia na uhamisho wa watu wanaohusika, na utaratibu wa kushughulikia malalamiko na kuongeza kuwa maafisa wake watawasilisha ripoti yao ifikapo mwezi Aprili mwaka huu.
Uchimbaji visima ulianza katikati ya 2023 na uzalishaji unatarajiwa kuanza mnamo 2025.