Pata taarifa kuu
Senegal-Uchaguzi

Wananchi wa Senegal wanaendelea kusherehekea ushindi wa Macky Sall

Wananchi wa Senegal waendelea kusherehekea ushindi wa Kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo ambae aliwahikuwa waziri mkuu, Macky Sall baada ya kushinda uchaguzi wa duri la pili uliofanyika jana nchini humo. vifijo na nderemo vinaendelea kusikika huku na kule jijini Dakar. Rais Abdoulaye Wade amekiri kushindwa uchaguzi huo na kumpongeza mpinzani wake kwa njia ya simu. Hatuwa ambayo inapongezwa na jamii ya kimataifa na ikimaanisha kukuwa kwa demokrasia na kwa wanasiasa nchini humo.

Wafuasi wa Macky Sall wakisherehekea ushindi wa kiongozi wao Jumapili 25.3.2012
Wafuasi wa Macky Sall wakisherehekea ushindi wa kiongozi wao Jumapili 25.3.2012 ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kuchaguliwa kwa Macky Sall kuiongoza Senegal kunamaanisha mwisho wa utawala wa miaka 12 ya rais Wade. Wafuasi wa Macky Sall walimiminika mabarabarani kusherehekea ushindi wa mfuasi wao huku wakiimba nyimbo za kumpongeza mshindi wao, wengine wakimtaja kuwa Macky Sall sasa ni rais.

Rais Abdoulaye Wade baada tu yakuona matokeo ya awali yakiendelea kutolewa alimpigia simu mpizani wake na kumpongeza huku akikubali kushindwa katika duru hiyo ya pili ya uchaguzi. msemaji wa rais Wade Serigne Mbacké Ndiaye alisema kuwa rais Wade amekubali maamuzi ya wananchi wa Senegal

Macky Sall mwenyewe muda mfupi baada ya Abdoulaye Wade kukiri kushindwa, alijitokeza kuwapongeza wale wote waliomchaguwa na wale ambao hawakumchaguwa, huku akisema kwamba uamuzi huo ni wawanchi wa Senegal.

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.

Viongozi wa kimataifa wamepongeza hatuwa hiyo iliofikiwa na Senegal. Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amewapongeza Abdoulaye Wade na Macky Sall, huku akiahidi kuendelea ushirikiano na uongozi mpya.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.