Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Marekani: Tuna imani kuwa Korea Kaskazini itawekewa vikwazo vipya

Marekani inasema ina matumaini kuwa Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa watapigia kura azimio ya kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini.

Donald Trump ameendelea kuishutumu Korea Kaskazini kwa kukataa kuacha majaribio yake ya silaha za nyuklia
Donald Trump ameendelea kuishutumu Korea Kaskazini kwa kukataa kuacha majaribio yake ya silaha za nyuklia REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivyo vipya, vinatarajiwa kupigiwa kura siku ys Jumatatu ijayo licha ya China na Urusi kuonekana kupinga azimio hilo.

Marekani inataka biashara ya mafuta kusitishwa kati ya mataifa mengine ya dunia na Korea Kaskazini na kuziwa kwa Mali za Kim Jong-un kutokana na nchi hiyo kuendelea kujaribu silaha zake za nyuklia.

Wakati huo huo rais wa Marekani Donald Trump amesema itakuwa ni siku ya huzuni kwa taifa la Korea Kaskazini ikiwa Marekani itaamua kuishambulia kijeshi.

Trump amesema kuwa hilo linawezekana kwa sababu Korea Kaskazini inaonesha tabia mbaya kwa kuendelea kujaribu silaha zake za nyuklia na kutishia usalama wake na ule wa dunia.

Marekani imeendelea kuishutumu Korea Kaskazini kwa kukataa kuacha majaribio yake ya silaha za nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.