Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Trump: Lazima Korea Kaskazini ipewe fundisho

Rais wa Marekani Donald Trump amesema itakuwa ni siku ya huzuni kwa taifa la Korea Kaskazini ikiwa Marekani itaamua kuishambulia kijeshi.

Wanaharakati mia tano waliweka vizuizi kwa msaada wa malori na matrekta ili kuzuia msafara wa magari ya kijeshi ya Marekani,Seongju, Septemba 7, 2017.
Wanaharakati mia tano waliweka vizuizi kwa msaada wa malori na matrekta ili kuzuia msafara wa magari ya kijeshi ya Marekani,Seongju, Septemba 7, 2017. Min Gyeong-seok/News1 via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Trump amesema kuwa hilo linawezekana kwa sababu Korea Kaskazini inaonesha tabia mbaya kwa kuendelea kujaribu silaha zake za nyuklia na kutishia usalama wake na ule wa dunia.

Marekani imeendelea kuishutumu Korea Kaskazini kwa kukataa kuacha majaribio yake ya silaha za nyuklia.

Hayo yakijiri siku ya Alhamisi jioni, Septemba 7, 2017, Korea Kusini ilikamilisha zoezi la kupeleka katika eneo lake kifaa chote cha mfumo wa kuzuia makombora kutoka Marekani, THAAD (Terminal High-Altitude Area Defense). Kifaa ambacho kimeelezwa muhimu, kwa sababu ya kuongezeka kwa tishio kutoka Korea Kaskazini. Zoezi hili limezua maandamano makubwa katika nchi jirani ya China, na maandamano makubwa nchini Korea Kusini.

Mfumo wa THAAD katika mji wa Seongju, Alhamisi, Septemba 7, 2017.
Mfumo wa THAAD katika mji wa Seongju, Alhamisi, Septemba 7, 2017. Lee Jong-hyeon/News1 via REUTERS

Makabiliano yaliendelea usiku mzima. Wanaharakati mia tano waliweka vizuizi kwa msaada wa malori na matrekta ili kuzuia msafara wa magari ya kijeshi ya Marekani yaliyokua yasafirisha vifaa hivyo vinnehadi katika ghuba ya Seongju, kusini-mashariki mwa Korea Kusini.

Polisi 8,000 hatimaye waliweza kuondoa vizuizi hivyo barabarani. Jumla ya watu 30 walijeruhiwa, kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Joongang.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.