Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Marekani yataka mali ya Kim Jong-un kuzuiliwa

Marekani inapendekeza kiongozi wa Korea Kaskazini, kuwekewa vikwazo zaidi na mali zake kuzuiwa, bila kusahau marufuku kwa biashara ya mafuta.

rais wa Marekani Donald Trump aendelea kumuonya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
rais wa Marekani Donald Trump aendelea kumuonya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un. ©SAUL LOEB, Ed JONES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Azimio hili litajadiliwa na kupigiwa kura na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Hatua hii imekuja baada ya Korea Kaskazini kuendelea kujaribu silaha zake za Nyuklia, suala ambalo Marekani imekuwa ikisema ni tishio kwa usalama wa dunia.

Iran ambayo pia inaaminiwa kuwa na silaha hizi imesema onyo la Marekani kwa Korea Kaskazini halikubaliki kwa sababu linatishia pia usalama wa dunia.

Hata hivyo China na Urusi zote zinatarajiwa kupinga vikwazo zaidi vipya.

Korea Kaskazini inadai kuunda bomu la haidrojeni na imekuwa ikitishia kuishambulia Marekani, hasa kisiwa cha Guam.

Korea Kaskazini tayari iko chini cha vikwazo vya kuitenga vilivyotangazwa na Umoja wa Mataifa, ambavyo vina nia ya kuulazimisha utawala wa nchi hiyo kusitisha mipango yake ya nyuklia.

Mwezi Agosti vikwazo vipya vya Umoja wa Mataifa vilipiga marufuku kuuzwa kwa mkaa wa mawe kutoka Korea Kaskazini ya thamani ya dola bilioni 1.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.