Pata taarifa kuu
UNSC-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana siku ya Jumatatu mjini New York ili kujaribu kutafuta suluhu katika mgogoro wa Korea Kaskazini. Wajumbe wa Baraza hilo walilaani kwa kauli moja jaribio la sita la Korea Kaskazini na kutoa wito wa kuchukuliwa vikwazo vpya wiki ijayo.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Korea Kaskazini, Septemba 4, 2017.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Korea Kaskazini, Septemba 4, 2017. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa ameilaumu Korea ya Kaskazini kwa kulazimisha vita kutokana na majaribio yake ya makombora ya mara kwa mara.

Nikki Haley ametaka kuwepo kwa muda wa dharura wa Baraza la Umoja wa Mataifa utakao jibu majaribio hayo kwa hatua kali.

Marekani inaonekana inataka kupendeza njia ya kidiplomasia kwa mzozo huo.

Miongoni mwa hatua ambazo zinaweza kupigiwa kura Jumatatu ijayo, kuna haja ya kuchukuliwa vikwazo vya mafuta, vikwazo vinavyolenga sekta ya utalii, makampuni ya kutengeneza nguo na wafanyakazi wa nje wa Korea Kaskazini.

Ulaya inaunga mkono mpango wa Marekani, amesema Francois Delattre, balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa: "Katika miezi michache, tishio limebadilika kwa ukubwa, hata kwa asili. Kwa sasa tishio ni la kimataifa. "

Marekani inataka kujadili wiki hii mzunguko wa nane wa vikwazo vya kupiga kura Jumatatu ijayo. Umoja wa Mataifa ulilipitisha tarehe 5 Agosti, vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Korea Kaskazini vinavyozuia dola bilioni moja vya mapato kwa kupiga marufuku mauzo ya nje ya makaa ya mawe, madini na bidhaa za uvuvi.

Siku ya Jumapili ilifanya jaribio la bomu la chini ya ardhi lililoaminika kuwa na nguvu ya kati ya kilotani 20 na 120.

Kifaa hicho hicho kinaweza kuwa na nguvu mara tatu zaidi ya bomu lililotumiwa kuharibu mji wa Hiroshima mwaka 1945.

Hata hivyo, China imesisitiza wito wake wa kutaka pande zote zirudi katika meza ya mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.