Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Japan na Marekani zafufua uhusiano wa karibu katika maswala ya ulinzi

Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida, waliyepokelewa kwa heshima katika Ikulu ya White House, wametangaza siku ya Jumatano ushirikiano wa karibu katika maswala ya ulinzi, ili kuimarisha zaidi uhusiano unaoelezewa kama "unastawi".

Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida wakiwa katika Ikulu ya White House.le 13 janvier 2023
Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida wakiwa katika Ikulu ya White House.le 13 janvier 2023 © Jonathan Ernst/AP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani, wakati wa mkutano na waandishi wa habari pamoja na mgeni wake, amekaribisha "maendeleo muhimu zaidi" katika ushirikiano wa nchi hizo mbili tangu kumalizika kwa Vita Baridi.

Mahasimu wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, majeshi ya Marekani na Japan kwa hiyo yatafanya kazi pamoja kwa ajili ya "kushirikiana" zaidi, huku Marekani ikijitolea kuunga mkono baadhi ya miradi ya kijeshi ya Japani, kwa kiwango cha vifaa na kiteknolojia.

"Kwa mara ya kwanza, Japan, Marekani na Australia zitaunda mtandao wa makombora ya anga na usanifu wa ulinzi," Joe Biden pia amesema, pia akitangaza mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya vikosi vya Japan, Marekani na Uingereza.

Bila kusahau kufanyika, siku ya Alhamisi mjini Washington, kwa mkutano wa kilele wa nchi tatu kati ya Japan, Ufilipino, na Marekani.

Nchi nyingi sana ambazo, pamoja na Korea Kusini, zinaunda mtandao wa ushirikiano ambao Joe Biden anaimarisha huko Asia, ili kukabiliana na matarajio ya China.

Mdemocrat huyo mwenye umri wa miaka 81, ambaye wakati huo huo anajitahidi kudumisha mazungumzo na Beijing, hata hivyo amesisitiza Jumatano, ni wazi kwa mamlaka ya China, kwamba uimarishaji wa muungano wa kijeshi na Tokyo ulikuwa "wa kujihami" tu.

Japan, ambapo wanajeshi wa Marekani wapatao 54,000 wanapiga kambi, ilirekebisha kimsingi fundisho lake la usalama wa kitaifa mwishoni mwa mwaka 2022, haswa ili kuwa na uwezo wa "kukabiliana na mashambulizi", licha ya Katiba yake ya amani.

Wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, Waziri Mkuu wa Japan ametoa wito wa "amani na utulivu" dhidi ya hali ya mvutano kati ya China na Taiwan.

- Mwezi na miti ya cherry -

Katika ishara nyingine ya ukaribu, Joe Biden pia aeahidi kwamba mwanaanga wa Japan atakuwa mtu wa kwanza asiye Mmarekani kutua Mwezini, kama sehemu ya misheni ya anga ya Marekani.

Akipokea mwenyeji wake kwa heshima za kijeshi asubuhi, Joe Biden alimsifu kiongozi "mwenye maono na jasiri" na akasifu muungano "usioweza kuharibika", na "unaostawi" kama miti ya micherry katika majira ya kuchipua.

Mnamo mwaka 1912, meya wa Tokyo alilipa kama zawadi jiji la Washington miti elfu kadhaa ya cherry, maua ambayo huleta watalii katika mji mkuu wa Marekani kila mwaka.

Fumio Kishida alifuata mfano huo, akionyesha kwamba nchi yake itatoa miti 250 ya ziada katika hafla ya kuadhimisha miaka 280 ya kuanzishwa kwa Marekani, mnamo 2026.

Viongozi hao wawili watajumuika jioni na wake zao, Jill Biden na Yuko Kishida, kwa chakula cha jioni.

Waziri Mkuu huyo mwenye umri wa miaka 66 ndiye kiongozi wa kwanza wa Japan kupokea heshima za ziara ya kiserikali mjini Washington tangu Shinzo Abe mwaka 2015.

Siku ya Alhamisi, Fumio Kishida atahutubia mabunge yote mawili ya Marekani kabla ya kupokelewa tena na Joe Biden, pamoja na Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos (mtoto wa dikteta wa zamani).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.