Pata taarifa kuu

O.J. Simpson, nyota wa zamani wa kandanda wa Marekani afariki

Mchezaji nyota wa zamani wa kandanda wa Marekani O.J Simpson, ambaye kesi yake ya mauaji ya mwaka 1995 ilivutia nchini Marekani kabla ya kuachiliwa huru, amefariki kutokana na saratani akiwa na umri wa miaka 76, familia yake imetangaza siku ya Alhamisi.

O.J. Simpson na dada yake Carmelita Durio (wa pili kutoka kushoto) wakiwasili kwa ajili ya hukumu ya kesi yake ya utekaji nyara na wizi huko Las Vegas katika Kituo cha Mahakama cha Kaunti ya Clark huko Las Vegas mnamo Oktoba 3, 2008.
O.J. Simpson na dada yake Carmelita Durio (wa pili kutoka kushoto) wakiwasili kwa ajili ya hukumu ya kesi yake ya utekaji nyara na wizi huko Las Vegas katika Kituo cha Mahakama cha Kaunti ya Clark huko Las Vegas mnamo Oktoba 3, 2008. REUTERS - POOL New
Matangazo ya kibiashara

"Mnamo Aprili 10, baba yetu, Orenthal James Simpson, alifariki kufuatia vita vyake na saratani," imeandika kwenye X familia ya mtu ambaye alichukuliwa kuwa mmoja wa nyota wa kwanza wakubwa weusi nchini Marekani.

Nyota wa zamani wa NFL, aliyeingia katika ulimwengu wa sinema, O.J Simpson alipatikana bila hatia ya mauaji ya mke wake wa zamani Nicole Brown na Ron Goldman, rafiki yake, huko Los Angeles mnamo mwaka 1995, wakati wa "kesi ya ya karne" iliyogongwa vichwa vya habari na iliyoshtumiwa kupita kiasi na kwa ubaguzi wa rangi. Mijadala hiyo ilivutia nchi na hukumu ya kumhukumu O.J Simpson inaendelea kuzua utata, karibu miaka 30 baadaye.

Mwaka mmoja kabla, msururu wa kasi ya chini kati ya makumi ya magari ya polisi na O.J Simpson pia ulikuwa umevutia Marekani.

"Siyo hasara kubwa kwa ulimwengu. Ni ukumbusho mwingine wa kifo cha Ron," babake Ron Goldman, Fred Goldman, aliambia NBC News kwa njia ya simu.

Gereza

O.J. Simpson alipatikana baadaye kuhusika na vifo vya wahanga hao wawili wakati wa kesi ya madai mwaka 1997 na kuamriwa kulipa fidia ya zaidi ya dola milioni 33 kwa familia zao, jambo ambalo hatawahi kufanya.

Mnamo 2007, alizungumziwa tena katika safu ya kisheria, alikamatwa huko Las Vegas kwa kuiba zawadi za michezo na watu watano kutoka kwa kasino ya hoteli jijini, kwa kuwatishia watu kwa bunduki. Mapema mwezi Oktoba 2008, alitiwa hatiani kwa makosa 12 kisha akahukumiwa kifungo cha miaka 9 hadi 33 jela. Aliachiliwa kwa dhamana tangu mwaka 2017.

Mnamo Februari, O.J Simpson alitangaza kwenye ukurasa wake wa X kwamba afya yake ilikuwa "nzuri" licha ya "matatizo fulani". "Nadhani itakuwa nyuma yangu hivi karibuni na ninatumai nitarejea kwenye uwanja wa gofu baada ya wiki mbili," alisema wakati huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.