Pata taarifa kuu

RDC:  Mwanahabari Stanis Bujakera ameachiwa huru kutoka gerezani

Nairobi – Mwanahabari mashuhuri wa DRC, Stanis Bujakera, hatimaye ameachiwa kutoka gerezani jana jioni baada ya kuwa kizuizini kwa zaidi ya miezi 6, mawakili na baadhi ya marafiki wamethibitisha.

Stanis Bujakera- Mwanahabari nchini DRC.
Stanis Bujakera- Mwanahabari nchini DRC. © Avec l'aimable autorisation de actualite.cd
Matangazo ya kibiashara

Bujakera, mwenye umri wa miaka 33, alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela Jumatatu ya wiki hii kwa madai ya kuhusika katika uandishi wa makala iliyotuhumu idara ya ujasusi ya jeshi kuhusika na mauaji ya mwanasiasa wa upinzani, Cherubin Okende.

Taarifa anayodaiwa kuandika, ilichapishwa katika jarida la Jeune Afrique na ilinukuu vyanzo kadhaa vya kijeshi, kabla ya mamlaka kujitokeza kudai kuwa sehemu kubwa ya tarifa ziliandikwa zilikuwa za kughushi.

Hata hivyo uamuzi wa mahakama, ulikashifiwa vikali na watetezi wa wanahabari waliodai kuwa tangu awali kesi dhidi yake ilionekana kuwa ni yakutengeneza, mawakili wake wakisema wanajipanga kukata rufaa.

Awali waendesha mashtaka walitaka mwanahabari huyo ahukumiwe kifungo cha miaka 20 jela, na huenda kuachiwa kwake kulitokana na shinikizo kutoka Serikalini baada ya majuma kadhaa nyuma, rais Felix tshisekedi kusema angefuatilia kesi ya mwanahabari huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.