Pata taarifa kuu

Nigeria: Hakuna kulipa kikombozi wa watekaji: Rais Tinubu

Nairobi – Rais wa Nigeria Bola Tinubu amewaagiza maafisa wa usalama kutotoa malipo yoyote au kikombozi kwa watekaji wa wanafunzi 250, tukio lililofanyika wiki iliyopita wakiwa shuleni katika kijiji cha Kuriga, jimboni Kaduna.

Matukio ya utekaji nyara wa wanafunzi yameongezeka nchini Nigeria.
Matukio ya utekaji nyara wa wanafunzi yameongezeka nchini Nigeria. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Msimamo huu wa serikali ya Nigeria unakuja wakati huu ndugu wa wanafunzi waliotekwa wakisema watekaji wamekuwa wakitaka kiwango kikubwa cha fedha kabla ya kuwaachia huru watoto wao.

Rais Tinubu amewaagiza maofisa wa usalama kuhakikisha raia waliotekwa wanaachiwa huru.

Kumeripotiwa ongezeko la visa vya utekaji nyara wa watu nchini humo katika kipindi cha wiki iliopita likiwemo tukio ambapo zaidi ya watu 60 walitekwa kutoka katika kijiji kimoja katika jimbo la Kaduna siku ya Jumanne.

Mamia ya wanafunzi nchini Nigeria wameripotiwa kutekwa katika kipindi cha miaka mitatu iliopita.

Baadhi ya mateka wameaachiwa huru baada ya kufanyika kwa mazungumzo na mamlaka japokuwa mamlaka inakana kulipwa kwa fidia.

Sheria iliopitishwa mwaka wa 2022 ilipiga marafuku ulipaji wa fidia kwa watekaji.

Ongezeko la matukio ya utekaji imekuwa changamoto kwa serikali ya rais Tinubu ambaye aliahidi kukabiliana na suala la ukosefu wa usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.