Pata taarifa kuu

Burkina Faso: Watu 170 wameuawa na wanajihadi: Waendesha mashtaka

Nairobi – Waendesha mashtaka nchini Burkina Faso, wamesema karibia watu 170 wameuawa katika mashambulio kwenye vijiji vitatu kaskazini mwa nchi hiyo wiki moja iliyopita, wanajihadi wa kiislamu wakinyooshewa kidole.

Watu walionusurika wanasema miongoni mwa waliouawa ni pamoja na wanawake na watoto.
Watu walionusurika wanasema miongoni mwa waliouawa ni pamoja na wanawake na watoto. RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa waendesha mashtaka, siku hiyo hiyo, Februari 25 katika mashambilio tofauti, wanajihadi hao walishambulia msikiti magharibi mwa nchi hiyo na kanisa moja kaskazini mwa burkina Faso, ambako dazeni ya watu waliuawa.

Mamlaka zinasema vijiji vilivyolengwa ni pamoja na Komsilga, Nodini na Soroe jimboni Yatenga, ambapo pamoja na kuua, walijeruhi watu, kuchoma nyumba moto na kuharibu miundombinu mingine.

Tayari wizara ya mambo ya ndani imeagiza uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo, watu walionusurika wakisema miongoni mwa waliouawa ni pamoja na wanawake na watoto.

Mashambulio ya wanajihadi yamesababisha vifo vya takriban watu elfu 20 na wengine zaidi ya milioni 2 kuhama makazi yao katika moja ya nchi maskini zaidi duniani iliyoko Sahel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.