Pata taarifa kuu

Equatoria Guinea: Mahakama yatoa hati ya kukamatwa Carmelo Ovono Obiang Nguema

Nairobi – Mahakama kuu nchini Uhispania, imekubali rufaa ya wanachama kadhaa wa upinzani nchini Equatoria Guinea, na kuagiza mahakama ya chini kutoa hati ya kukamatwa kwa mtoto wa rais wa nchi hiyo, Carmelo Ovono Obiang Nguema.

Carmelo Ovono Obiang Nguema ni mtoto wa kiume wa rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo
Carmelo Ovono Obiang Nguema ni mtoto wa kiume wa rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo REUTERS - DAVID MERCADO
Matangazo ya kibiashara

Carmelo na maafisa wengine wawili waandamizi walishtakiwa kwa kuwateka nyara wanachama wanne wa kundi la upinzani lenye makao yake nchini Uhispania, walipokuwa safarini kwenda Sudan Kusini mwaka 2019.

Awali mahakama hiyo ilitangaza kuwa imeanza kumchunguza tangu kutolewa kwa madai hayo, ambayo Wadadisi walisema huenda yakaharibu juhudi za rais huyo kuboresha sifa yake kimataifa.

Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, ametawala koloni hilo la zamani la Uhispania lenye utajiri mkubwa wa mafuta tangu 1979, na amekuwa akijipatia ushindi kwenye chaguzi kadhaa za nchi hiyo, na sasa yuko madarakani kwa muhula wa sita

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.