Pata taarifa kuu

Ethiopia: IGAD inasema ina matumaini mazungumzo ya amani yatarejelewa

Nairobi – Jumuiya ya kikanda ya nchi za Afrika Mashariki na pembe ya Afrika, IGAD, hapo jana ilisema bado ina matumaini kuhusu mazungumzo zaidi kati ya Serikali ya Ethiopia na wapiganaji wa eneo la Oromo, licha ya mazungumzo yaliyofanyika Tanzania juma hili kukwama.

Mazungumzo yaliyofanyika Tanzania juma hili kati ya serikali ya Ethiopia na waasi wa Oromo yamekosa kupata muafaka
Mazungumzo yaliyofanyika Tanzania juma hili kati ya serikali ya Ethiopia na waasi wa Oromo yamekosa kupata muafaka © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya IGAD imekuja baada ya mazungumzo ya raundi ya tatu kati ya Addis Ababa na viongozi wa eneo la Oromia, kushindwa kupata muafaka licha ya uungwaji mkono wa jumuiya za kikanda na ile ya kimataifa.

Kila upande unamtuhumu mwingine kwa kukwamisha mchakato wa maridhiano unaolenga kujaribu kumaliza vita iliyodumu kwa karibu miaka 5, ikihusisha mauaji ya kikabila.

Katibu mkuu wa IGAD, Workneh Gebeyehu, ametoa wito kwa pande zinazohusika kuonesha uwajibikaji katika mchakato wa amani, akiwataka viongozi kuweka mbele maslahi ya raia.

Kwa muda sasa Serikali ya waziri mkuu Abiy Ahmed, imekuwa ikiwatuhumu waasi wa Oromia kwa mauaji, tuhuma ambazo hata hivyo viongozi wa eneo hilo wameendelea kukanusha wakidai Serikali kutekeleza mashambulio ya kupanga dhidi ya wapinzani wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.