Pata taarifa kuu

Guinea: Moussa Dadis Camara, mkuu wa zamani wa mapinduzi ya kijeshi, arejeshwa gerezani

Moussa Dadis Camara amerejea gerezani, wakili wake ametangaza siku ay Jumamosi, Novemba 4 mchana. Rais wa zamani wa Guinea, aliyezuiliwa katika Ikulu Kuu ya Conakry kwa zaidi ya mwaka mmoja, alitotoroshwa katika gereza alikokuwa anazuiliwa asubuhi ya Jumamosi muda mfupi kabla ya mapambazuko na kundi la watu waliokuwa awmejihami kwa silaha nzito.

Moussa Dadis Camara, kiongozi wa Guinea wakati wa mauaji ya Septemba 28, 2009 huko Conakry, akizungumza mahakamani wakati wa kesi yake Septemba 28, Desemba 12, 2022.
Moussa Dadis Camara, kiongozi wa Guinea wakati wa mauaji ya Septemba 28, 2009 huko Conakry, akizungumza mahakamani wakati wa kesi yake Septemba 28, Desemba 12, 2022. © LAMARANA DJEBOU SOW / AFPTV
Matangazo ya kibiashara

Tangu alipotoroshwa kutoka jela aanakozuiliwa Jumamosi asubuhi, Moussa Dadis Camara alikuwa akitafutwa katika mji mkuu, uliokuwa umezingirwa na vikosi vya ulinzi na usalama. Kulingana na wakili wa Dadis Camara, haikuwa kutoroka, bali utekaji nyara.

Wakili huyo ameielezea RFI kwamba rais huyo wa zamani aliamshwa ghafla akiwa usingizini, kabla ya watu waliokuwa na silaha kumuondoa kwa nguvu kutoka kwenye jela alikokuwa anazuiliwa pamoja na wafungwa wenzake watatu, Kanali Moussa Tiegboro Camara, Kanali Claude Pivi na jenerali Blaise Goumou.

Wote wamekuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja, angalau, na wote wanakabiliwa na mashtaka kwa madai ya kuhusika katika mauaji ya Septemba 28, 2009 ambayo yalisababisha vifo vya karibu watu 160 na ubakaji wa karibu wanawake mia moja.

Kulingana na mwanasheria wake Lamah, Dadis Camara alitekwa nyara na kundi hili lenye silaha. Aliweza kuongea na mteja wake kwa njia ya simu ambaye alimweleza kuwa alifanikiwa kuwatoroka watu wanaodaiwa kumteka, kabla ya kurudi gerezani, hata kama wakili huyo hakutaka kueleza kwa undani mazingira halisi ambayo mkuu huyo wa zamani wa utawala wa kijeshi wa CNDD aliweza kurejea katika jela kuu.

Kanali Tiegboro, ambaye pia aliachiliwa kutoka gerezani, pia alimwambia wakili wake kwamba alikuwa amewahadaa watekaji wake, kabla ya kuwaacha na kurudi katika gereza alikokuwa anazuiliwa.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Mkuu wa Majeshi hathibitishi matoleo haya mawili na badala yake anadai "kukomesha utoro huo" kwa wafungwa na amehakikishia kwamba "hatua zote za usalama zimechukuliwa ili kupata mfungwa wa mwisho aliyetoroka. , Claude Pivi ".

Operesheni zitaendelea. Ni muhimu kuviacha vyombo vya usalama vifanye kazi yao. Operesheni hiyo iliyopelekea kuwapata wengine,  itaendelea kwa sababu lengo katika yote haya ni kwamba kesi ya matukio ya Septemba 28 ni ahadi kutoka kwa serikali ya rais wa Jamhuri ambaye, katika sera yake ya kutoa adhibu, kupitia Waziri wa Sheria, ameweka vita dhidi ya kutokujali kuwa kitovu cha matatizo yake kama sehemu ya ujenzi wa Taifa. Nina matumaini mazuri na kwa vyovyote vile nina imani kwamba atapatikana hivi karibuni. Uchunguzi unaoendelea utafanya iwezekane kubaini wahalifu, kilichoanzishwa rasmi ni kwamba watu hao waliokuwa na silaha nzito walivamia jela kuu la Conakry kwa lengo moja la kuwaondoa Kapteni Moussa Dadis Camara, Tiegboro, Blaise Goumou na Bw. Claude Pivi, amesema Alphonse Charles Wright, Waziri wa Sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.