Pata taarifa kuu

Karibia watu 37 wameuawa katika shambulio la Boko Haram nchini Nigeria

Wapiganaji wenye itikadi kali kaskazini mashariki mwa Nigeria wamewauwa takriban wanakijiji 37 katika mashambulio mawili tofauti, kwa mujibu wa wakaazi katika maeneo hayo.

Serikali ya Nigeria imekuwa ikipambana na wapiganaji wa kundi la Boko Haram kaskazini mashariki ya taifa hilo kwa muda sasa
Serikali ya Nigeria imekuwa ikipambana na wapiganaji wa kundi la Boko Haram kaskazini mashariki ya taifa hilo kwa muda sasa AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji hao wenye itikadi kali waliwalenga wanakijiji katika wilaya ya Geidam katika jimbo la Yobe siku ya Jumatatu na Jumanne katika shambulio la kwanza katika jimbo hilo katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja.

Awali watu hao wenye silaha waliwaua kwa risasi watu 17 kabla ya kuwaua wengine 20 kwa kutumia kilipuzi wakati wakihudhuria mazishi.

Kundi la Kiislamu la Boko Haram lilianzisha uasi kaskazini mashariki mwa Nigeria mwaka 2009 katika juhudi za kuanzisha matumzi ya kanuni zao katika eneo hilo.

Takriban watu 35,000 wameuawa na zaidi ya milioni 2 kukimbia makazi yao kutokana na ghasia katika jimbo la Borno, ambalo ni jirani na Yobe.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu, ambaye aliingia madarakani mwezi Mei, hajafaulu kumaliza mizozo ya usalama katika taifa hilo katika maeneo ya kaskazini mashariki na kaskazini-magharibi na kati ambapo makumi ya makundi yenye silaha yamekuwa yakiua wanavijiji na kuwateka nyara wasafiri ili kuwalipa fidia.

Serikali ya jimbo la Yobe siku ya Jumatano iliitisha mkutano wa dharura wa usalama kuhusu mashambulio hayo ambayo ililaumu watu wenye itikadi kali walioingia katika jimbo hilo kutoka jirani na Borno.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.