Pata taarifa kuu

DRC: Awamu inayofuata ya mchakato wa Nairobi kufanyika Novemba 16

Kikao kijacho cha Mchakato wa Nairobi kitaanza Novemba 16 jijini Nairobi, Kenya. Tangazo hilo limetolewa mwishoni mwa wiki hii katika taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). 

Rais wa zamani wa Kenya na Mpatanishi wa EAC, Uhuru Kenyatta (wa pili kulia) na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi (kushoto) wakiangalia uwakilishi mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye ramani baada ya kutia saini mkataba wa kuijumuisha DRC katika jumuiya ya kibiashara ya Afrika Mashariki, jijini Nairobi mnamo Aprili 8, 2022.
Rais wa zamani wa Kenya na Mpatanishi wa EAC, Uhuru Kenyatta (wa pili kulia) na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi (kushoto) wakiangalia uwakilishi mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye ramani baada ya kutia saini mkataba wa kuijumuisha DRC katika jumuiya ya kibiashara ya Afrika Mashariki, jijini Nairobi mnamo Aprili 8, 2022. AFP - TONY KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo inasema uamuzi huo umechukuliwa baada ya mashauriano yaliyoongozwa na Rais wa Burundi na Mwenyekiti wa sasa wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za EAC. Aidha alisisitiza haja ya kudumisha ushirikishwaji kwa kuhakikisha ushiriki wa wadau wote na kubainisha kuwa vikao vyote hivi sasa vitajumuisha viongozi mbalimbali wa jumuiya.

Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za EAC na Rais wa Burundi, Évariste Ndayishimiye, aliongoza Ijumaa mjini Bujumbura mashauriano na Mpatanishi wa EAC, Rais Uhuru Kenyatta, kuhusu hali ya usalama kwa sasa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Walipitia maendeleo yaliyopatikana katika utekelezaji wa safu za siasa na kijeshi, zilizopangwa kuleta utulivu Mashariki mwa DRC.

Walibainisha kuwa wakati zoezi la kutuma kikosi hicho unaendelea, mkondo wa kisiasa unaimarishwa kuelekea suluhisho la kina kwa hali ya usalama ya muda mrefu.

Mkutano huo pia ulitoa wito kwa makundi yote ya kigeni yenye silaha kurejea katika nchi zao za asili bila masharti.

Wakati wa mkutano huu, mambo kadhaa yaliafikiwa kwa ajili ya utekelezaji wa mkondo wa kisiasa, kuelekea suluhisho la kudumu la amani na usalama mashariki mwa DRC. Alihimiza kuendelea kwa ushirikiano kati ya mchakato unaoongozwa na EAC na mchakato wa Luanda ili kupunguza mvutano kati ya mataifa ndugu ya DRC.

mbali na hayo, kikao cha mashauriano kilizishukuru nchi za Burundi, Kenya na Uganda kwa kupeleka wanajeshi haraka na kuzitaka nchi nyingine zinazochangia wanajeshi kuharakisha kutuma wanajeshi wao ndani ya muundo na mfumo uliokubaliwa.

Rais wa Burundi pia alithibitisha kuwa alikuwa na mazungumzo na wakuu wote wa nchi za Jumuiya juu ya kupitishwa kwa mbinu ya kikanda, ndani ya mfumo uliokubaliwa, kusimamia hali na kujenga imani kati ya nchi wanachama wa EAC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.