Pata taarifa kuu

Rwanda imeondoa ulazima wa uvaaji barakoa katika maeneo ya umma.

Nchi ya Rwanda, imetangaza kulegeza baadhi ya sheria zilizokuwepo za kudhibiti msambao wa Uviko 19 .Sharti la uvaaji barakoa katika maeneo ya umma likiondolewa

Raia wa Rwanda akipokea chanjo ya Uviko 19 jijini Kigali.
Raia wa Rwanda akipokea chanjo ya Uviko 19 jijini Kigali. © REUTERS/Jean Bizimana
Matangazo ya kibiashara

Rwanda ni mojawapo wa mataifa ya bara Afrika ambayo  yamekuwa yakitoa chanjo ya uviko 19 kwa raia wake kwa kasi, idadi kubwa ya raia wake wakiwa tayari wamechoma chanjo kikamilifu .

Licha ya kuondolewa kwa ulazima wa uvaaji barakoa, raia watahitajika kuwa wamechoma chanjo kikamilifu kabla ya kuruhiswa kuingia katika majengo ya serikali pamoja na kutumia usafiri wa umma kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ofisi ya waziri mkuu.

Rwanda imetajwa kuwa na mpango bora wa kabiliana na maambukizi ya uviko 19 ikiwa imesajili vifo 1,459 tangu kuaanza kwa janga hilo duniani.

Baadhi ya mataifa ya ulimwengu yameendelea kulegeza baadhi ya marsharti ya kabiliana na uviko 19, Ufaransa ikiwa taifa la hivi punde barani ulaya kuondoa ulazima wa uvaaji barakoa katika maeneo ya umma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.