Pata taarifa kuu
EQUATORIAL GUINEA-SIASA

Equatorial Guinea: Rais Obiang kuwania kiti cha urais kwa muhula wa 6

Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, ambaye anashikilia rekodi ya dunia ya maisha marefu ya kuwa rais ambaye bado yuko hai na rais akiwa madarakani kwa miaka miaka 42, bila kujumuisha utawala wa kifalme, kuna uwezekano mkubwa ateuliwe katika kongamano la chama chake siku ya Jumanne kuwania muhula wa sita katika uchaguzi wa mwaka 2023.

Bw. Obiang, ambaye alichukua mamlaka kupitia mapinduzi mwaka wa 1979 na kutawala nchi kwa mkono wa chuma, alikuwa ameondolewa katika ulingo wa kisiasa kwa miezi kadhaa kwa niaba ya Teodorin, 53.
Bw. Obiang, ambaye alichukua mamlaka kupitia mapinduzi mwaka wa 1979 na kutawala nchi kwa mkono wa chuma, alikuwa ameondolewa katika ulingo wa kisiasa kwa miezi kadhaa kwa niaba ya Teodorin, 53. AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Wiki chache zilizopita hata hivyo, mtoto wake wa kiume Teodoro Nguema Obiang Mangue, anayejulikana na kwa jina la Teodorin, alionekana kuteuliwa kwenye nafasi hiyo badala yake, taarifa ambayo ilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii.

Chama cha Democratic Party of Equatorial Guinea (PDGE), chama kimoja hadi mwaka 1991, kitafanya Kongamano lake la 7 Jumatatu na Jumanne huko Bata, mji mkuu wa kiuchumi. Kongamano hili la mwisho la kawaida kabla ya uchaguzi litamteua mgombea wa urais katika uchaguzi wa mwaka 2023 kwa muhula wa miaka 7.

Bw. Obiang, ambaye alichukua mamlaka kupitia mapinduzi mwaka wa 1979 na kutawala nchi kwa mkono wa chuma, alikuwa ameondolewa katika ulingo wa kisiasa kwa miezi kadhaa kwa niaba ya Teodorin, 53.

Teodorin kwa muda mrefu amekuwa akioneshwa kama mrithi wake, makamu wa rais wa Jamhuri na naibu kiongozi wa chama cha PDGE, aambaye alionekana hadharani kila sehemu hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.