Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

DRC: Kambi ya Kabila yapinga utaratibu wa kuidhinisha maafisa wa CENI

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kambi ya rais wa zamani Joseph Kabila imekataa kushiriki katika kamati ya pamoja ambayo inatarajia kuchunguza wagombea kweye nafai ya mwenyekiti wa Tume mpya ya Uchaguzi (CENI).

Emmanuel Ramazani Shadary, kutoka muungano wa FCC, na kiongozi wa chama cha kisiasa cha Joseph Kabila, PPRD, Agosti 13, 2021.
Emmanuel Ramazani Shadary, kutoka muungano wa FCC, na kiongozi wa chama cha kisiasa cha Joseph Kabila, PPRD, Agosti 13, 2021. © Pascal Mulegwa/RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake Jumamosi, Agosti 14, Spika wa Bunge ametangazaameongza muda wa "nyongeza wa saa 72" kwa madhehebu ya kidini "ili kufikia makubaliano juu ya uteuzi wa mwenyekiti wa CENI. "

Kambi inayounga mkono Joseph Kabila, FCC, haina mpango wa kushiriki katika kamati ya pamoja na imemwarifu Spika wa Bunge la Kitaifa. Inahitaji majadiliano ili kupata makubaliano kati ya wadau wote. Hivi ndivyo alivyosema Emmanuel Ramazani Shadary, kutoka FCC na kiongozi wa chama cha PPRD, chama cha Rais wa zamani Joseph Kabila.

"Hatuungi mkono mchakato huu ambao hauna makubaliano katika uchaguzi wa maafisa wa CENI. Kwa kamati ya pamoja, sasa tunaona kwamba kweli kuna nia ya wazi ya kutuongoza kuelekea kwenye udikteta kwa lengo la mabadiliko.

"Ikiwa wameunda kamati ya pamoja, upinzani unaoongozwa na FCC hautashiriki. Hii ni kamati iliyo kinyume cha sheria na isiyo na maana. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.