Pata taarifa kuu
SUDAN-HAKI

Sudan: Maswali yaibuka kuhusu kutumwa kwa Omar Bashir kwenda ICC

Sudan na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) walitia saini Alhamisi, Agosti 12 huko Khartoum makubaliano ya ushirikiano, ambayo yanaweza kufungua njia ya kumkabidhi rais wa zamani wa nchi hiyo Omar al-Bashir na washirika wake kwa mahakama hii.

Rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir, hapa ilikuwa Aprili 5, 2019 huko Khartoum.
Rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir, hapa ilikuwa Aprili 5, 2019 huko Khartoum. © REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Karim Khan, mwanasheria mkuu wa ICC, hati hii mpya ya makubaliano iliyosainiwa na serikali ya Sudan inapaswa kujumuisha wale wote ambao wanakabiliwa na waranti wa kimataifa wa kukamata vilivyotolewa na ICC. Lakini bado serikali inasita kabla ya al-Bashir kukabidhiwa kwa Mahakama ya  Kimataifa ya Jinai (ICC).

Baada ya idhini kutoka kwa serikali ya Sudan, Baraza kuu la muda litalazimika kutoa idhini yake. litamua ikiwa linakubali au la kumkabidhi rais Omar al-Bashir na maafisa wawili wa zamani wa utawala wake kwa ICC.

Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi wiki hii, Karim Khan alisema uamuzi huo utachukuliwa katika mkutano wa Baraza kuu la Muda na serikali. Lakini bado hakuna tarehe maalum ya mkutano huu, na mwanasheria mkuu wa ICC alikiri kwamba hakupewa tarehe rasmi kutoka kwa mamlaka ya Sudan ambayo Bashir atafikishwa ICC. Kulingana na mmoja wa mawakili wa al-Bashir, "halitakuwa jambo rahisi".

Tangu Jumatano, Agosti 11, suala hili limeibua maswali mengi. Jeshi bado linasita kumkabidhi al-Bashir kwa mahakama ya ICC. Raia wa Sudan kwa upande wao waliona uamuzi huu kama udhalilishaji wa Sudan na wanaomba rais wa zamani wa Sudan ahukumie na vyomvo vya sheria vya Sudan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.