Pata taarifa kuu
NIGER- UCHAGUZI

Uchaguzi wa rais Niger: waangalizi wametoa wito kwa wagombea kuheshimu matokeo

Waangalizi kutoka Jumuiya ya Mataifa ya Sahelo-na Sahara CEN-SAD Jumatatu ya tarehe 22 mwezi wa february wamewataka wagombea wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais uliofanyika siku ya Jumapili nchini Niger kuheshimu matokeo ya sanduku la kura, wito ambao umetolewa wakati mgombea urais wa chama tawala humo, Mohamed Bazoum akiendelea kuongoza dhidi ya mpinzani wake Mahamane Ousmane.

Mgombea wa uchaguzi Niger Bazoum Mohammed na mpinzani wake Mahamane Ousmane 2019.
Mgombea wa uchaguzi Niger Bazoum Mohammed na mpinzani wake Mahamane Ousmane 2019. RFI Hausa
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo wa waangalizi wa jumuia hiyo CEN-SAD uliwahimiza wagombea wote katika kinyang'anyiro hicho kuheshimu matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi yakiendelea kutangazwa, na kuwataka kutumia njia za kisheria kumaliza tofauti zao za kisiasa.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo alisema kuwa kati ya majimbo 266 tayari matokeo kutoka majimbo 196 yameshatangazwa na kwamba Mohamed Bazoum anaongoza kwa asilimia 52.9 bila ya kutoa maelezo zaidi.

Wakati huu matokeo yakiendelea kutangazwa, Nassirou Bako mwenyekiti wa shirika la CEN-SAD lililoangazia uchaguzi huo, amefahamisha kuwa uchaguzi huo ulifanyika katika mazingira yaliyo tulivu katika baadhi ya maeneo tofauti na maeneo yaliyoshuhudia vifo vya maafisa saba wa tume ya uchaguzi.

Nassirou Bako ,Mwenyelkiti wa Shirika la CEN-SAD, lililoshiriki katika uangalizi wa Uchaguzi wa marudio nchini Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.