Pata taarifa kuu
DRC-ADF-USALAMA

Beni: Watu 21 wauawa na watoto kadhaa watekwa nyara na waasi wa ADF

Watu ishirini na moja wameuawa, wengine wanne wamejeruhiwa na watoto kadhaa wametekwa nyara katika mashambulizi mawili ya ADF usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano Novemba 20 katika mji wa Beni na wilaya ya vijijini ya Oicha, mji mkuu wa Beni, kwa mujibu wa Radio Okapi.

Askari wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakisimama karibu na silaha kubwa ya kurusha roketi nyingi kwa wakati mmoja huko Matombo, kilomita 35 kaskazini mwa Beni, Kivu Kaskazini, Januari 13, 2018.
Askari wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakisimama karibu na silaha kubwa ya kurusha roketi nyingi kwa wakati mmoja huko Matombo, kilomita 35 kaskazini mwa Beni, Kivu Kaskazini, Januari 13, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya raia yameripoti vifo saba katika mji wa Beni. Idadi hii imethibitishwa na vyanzo vingine vya usalama ambavyo vimesema kuwa askari wawili wa DRC, FARDC, pia wamejeruhiwa wakati wa mapigano.

Leo Jumatano, makundi ya vijana yameandamana katika mji wa Boikene, huku wakiweka vizuizi kwenye barabara kuu, wakiomba jeshi la DRC ( FARDC), polisi na kikosi cha Umoja aw Mataifa nchini humo (MONUSCO) kuwalindia raia usalama wao.

Pia usiku wa kuamkia leo Jumatano, waasi wa ADF walifanya shambulio jingine katika eneo la Mavete katika wilaya ya vijijini ya Oicha. Vyanzo vya usalama vimeripoti kuwa raia watatu wameuwa, lakini mashirika ya kiraia yametoa idadi ya watu 14 ambao wameuawa katika shambulio hilo.

Mashirika hayo ya kiraia yanabaini kwamba yametahadharisha kuwa waasi wa ADF wamepenya na kuingia katika maeneo kadhaa ya mji wa Beni wakati jeshi la FARDC lilikuwa likiendesha mashambulizi dhidi ya kundi hilo.

Shambulio hili ni la kwanza la ADF katika mji wa Beni tangu Oktoba mwaka wa 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.