Pata taarifa kuu
ICGLR_USALAMA

Wakuu wa majeshi ya ukanda wa Maziwa Makuu wajadili kuhusu usalama katika nchi zao

Wakuu wa Majeshi kutoka mataifa ya Maziwa makuu wanakutana mjini Goma Mashariki mwa DRC, kujadili mipango na mbinu ya kuimarisha usalama katika mataifa hayo.

Makao makuu ya Jiji la Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 2016.
Makao makuu ya Jiji la Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 2016. RFI/Leonora Baumann
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la DRC, Jenerali Leon-Richard Kasonga, amesema wakuu hao kutoka Burundi, Rwanda, Tanzania, Uganda na DRC hawajadili tu utovu wa usalama Mashariki mwa DRC lakini pia wanaangazia namna ya kuimarisha usalama katika mataifa yao.

Mkutano huo unatarajaiwa kumalizika leo.

Mkutano kama huo ulifanyika Mwezi Agosti 2012 katika mji huo wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kumalizia mikakati ya kuunda jeshi la pamoja lililokwenda Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupambana na waasi wa M23.

Viongozi hao walikutana katika mji wa Goma baada ya makubaliano ya marais wa mataifa 11 ya Maziwa Makuu waliokutana jijini Kampala Uganda kujadili namna ya kukabiliana na waasi wa M 23.

Wadadisi wanaona kwamba mkutano una wakati muafaka, baada ya viongozi wa DRC kuthibitisha kwamba eneo la mashariki linakabiliwa na mdororo wa usalama hasa katika maeneo ya Beni na Rutshuru, katika mkoa wa Kivu Kusini na katika eneo la Minembwe na maeneo mengine ya Bonde la Ruzizi na Fizi, katika mkoa wa Kivu Kusini.

Mapema wiki hii tume ya Umoja Mataifa nchini DRC, MONUSCO, ilipendekeza kuanzishwa kwa operesheni ya kuwapokonya silaha wapiganaji wanaowakilisha makabila yao katika eneo hilo.

Jeshi la DRC limeyataka makundi yanayopigana katika eneo la Minembwe, Fizi na katika bonde la Ruzizi kukubali kuweka silaha chini, kauli ambayo imetolewa wakati huu juhudi za kuyapatanisha makabila yanayozozana kwenye maeneo hayo zikiendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.