Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-WANAJESHI-ABIY

Wanajeshi nchini Ethiopia wafungwa jela

Mahakama ya kijeshi nchini Ethiopia, imewafunga jela wanajehi 66 kati ya miaka 5 na 14 jela baada ya kuandamana kwenda katika ofisi ya Waziri Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed REUTERS/Kumera Gemechu
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao, walikuwa wanaandamana wakitaka nyongeza ya mshahara, na Waziri Mkuu Abiy Ahmed alionekana akikutana na wanajeshi hao katika ofisi yake na hata kushirikiana nao kufanya mazoezi.

Ahmed amewahi kunukuliwa akisema kuwa, wanajeshi hao walipanga kumuua.

Waziri Mkuu Abiy ameendelea kupongezwa kimataifa kwa mageuzi anayoyafanya nchini humo tangu kuingia madarakani mwezi Aprili mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.