Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Felix Tshisekedi arejea Kinshasa katika hali ya mvutano

Chama cha upinzani ch UDPS kimeghadhabishwa na hatuwa iliochukuliwa na serikali ya DR Congo ya kuwazuia wafuasi wa chama hicho kwenda kumlaki kwa wingi kiongozi wa chama hicho Felix Tshisekedi aliewsili jana Jumapili jijini Kinshasa akitokea ziarani barani Ulaya.

Félix Tshisekedi alipokelewa kwenye uwanja wa ndege wa Kinshasa na baadhi ya wajumbe wa vyama vya upinzani. (Picha ya zamani).
Félix Tshisekedi alipokelewa kwenye uwanja wa ndege wa Kinshasa na baadhi ya wajumbe wa vyama vya upinzani. (Picha ya zamani). ERIC LALMAND / Belga / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ilitarajiwa kwamba kiongozi huyo angelipata mapokezi makubwa kutoka kwa wafuasi wa chama hicho, lakini sivyo ilivyokuwa na badala yake amepokkelewa na watu kadhaa kutoka chama hicho ambao ni vingozi wa ngazi za juu wa UDPS.

Polisi ya zima ghasia nchini DR Congo ndio waliomsindikiza kutoka uwanja wa ndege wa Njili jijini Kinshasa hadi nyumbani kwake, ambako taarifa zinaeleza kuwa baadae nyumba hiyo ilizingirwa.

Jean Marc Kabund, katibu mkuu wa chama hicho cha upinzani cha UDPS anasema kwamba haikubaliki kuona haki ya msingi ya wananchi inaendelea kukandamizwa.

Katika hatuwa nyingine, polisi katika maeneo kadhaa hususan mjini Bukavu jimboni Kivu ya Kusini, Lumbumbashi pamoja na Luanda mgharibi mwa nchi hiyo ambako Martin Fayulu kiongozi wa upinzani ambae alizuiliwa na Polisi kuwakusanya wafiasi wake na kualazimika kuelekea eneo la Boma, ambako pia alizuiliwa.

Hayo yakijiri, Denis Mukwege, daktari maarufu katika kutoa huduma kwa wanawake waliokumbwa na janga la ubakaji ambae you ziarani nchini Ufaransa amekutana na raia wa DR Congo wanaoeshi ugenini amesema bado ni mapema mno kuzungumzia kuwania urais kabla ya kuzungumzia kufanikisha mchakato wa kufanyika kwa uchaguzi.

Daktari huyo aliejipatia umaaarufu hadi kupewa tuzo, amesema wanachowania sio madaraka, bali ni kuhakikisha utawala wa kisheria, na uhuru wa kujitetea na kwamba hajafikria kuwania urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.