Pata taarifa kuu
DRC-MONUSCO

Ofisi za MONUSCO zavamiwa mkoani Kasai nchini DRC

Tume ya umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO imelaani kile inachosema ni uvamizi uliofanywa kwenye ofisi zake zilizoko kwenye mkoa wa Kasai na wanajeshi wa Serikali.

Wanajeshi wa MONUSCO nchini DRC
Wanajeshi wa MONUSCO nchini DRC Photo Monusco/Michael Ali
Matangazo ya kibiashara

Hapo jana kundi la wanajeshi wa Serikali lililazimisha kuingia kwenye eneo la ofisi za MONUSCO mjini Kananga, kwa kile wanajeshi hao walidai wanamsaka mwandishi wa habari wa nchi hiyo aliyeifika hapo kuomba hifadhi.

Mjumbe maalumu wa umoja wa Mataifa Maman Sidikou ameeleza hatua ya wanajeshi hao kama tukio la kuogofya, akisema wanajeshi hao walipokea amri kutoka kwa afisa mmoja wa juu wa jeshi aliyeagiza kuzingirwa kwa ofisi hizo.

Sidikou ameitaka Serikali kuheshimu sheria za kimataifa na mikataba iliyotia saini na kuwachukulia hatua wanajeshi walioshiriki kwenye operesheni hiyo huku akisisitiza kuheshimiwa kwa uhuru wa vyombo vya habari.

Wanajeshi hao walikuwa wanamsaka mwanahabari Eduard Diye Tshitenge aliyekuwa awasilishe ilani yake juma hili kuhusu kushinikiza kuondoka madarakani kwa rais Josephu Kabila.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.