Pata taarifa kuu
UN-DRC-MONUSCO-USHIRIKIANO

Umoja wa Mataifa kuamua juu ya hatma ya MONUSCO

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unazuru nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuangalia kuhusu hatma ya kikosi cha kulinda amani Monusco baada ya kupunguzwa kwa bajeti ya kikosi hicho kwa asilimia 8 ambapo watakuwepo nchini humo hadi Agosti 7 mwaka huu.

Kwenye makao Makuu ya MONUSCO, Kinshasa, DR Congo.
Kwenye makao Makuu ya MONUSCO, Kinshasa, DR Congo. Photo Monusco/Michael Ali
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo wa watu zaidi ya 20 wanajeshi na raia wa kawaida, unaongozwa na El Ghassim Wane, raia wa Mauritania ambae ni naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anaehusika na operesheni za vikosi vya kulinda amani kwenye Umoja huo.

Wajumbe hao wa Umoja wa Mataifa watakutana na pande mbalimbali nchini humo kuangalia hasa hatma ya MONUSCO, ambayo imeshuhudia hivi karibuni bajeti yake ikipunguzwa kwa asilimia 8%.

Akizungumza na vyombo vya habari hapo jana baada ya kukutana na viongozi wa serikali, kiongozi wa ujumbe huo amesema swali tete ni kutotekelezwa kikamilifu kwa makubaliano ya desemba 31.

Utekelezaji wa makubaliano hayo ni moja ya masharti yaliyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kabla ya kuzingatia mkakati kuondolewa kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini humo, jambo ambalo laonekana kuwa mbali kidogo kutokana na kuendelea kwa mgogoro wa kisiasa na kiuchumi.

Baada ya kukamilisha ziara hiyo nchini DR Congo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaehusika na operesheni za kulinda amani atawasilisha ripoti kwenye Baraza la Usalama la Umoja huo pamoja na mapendekezo kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.