Pata taarifa kuu
TANZANIA-KASHFA YA MCHANGA

Tanzania: Rais Magufuli kupokea ripoti ya pili ya uchunguzi mchanga wa madini

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli hii leo anatarajia kupokea ripoti ya kamati ya pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi wa madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga wa madini yaliyopo maeneo mbalimbali nchini humo.

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli akikagua ripoti ya tume aliyounda kuhusu mchanga wa madini.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli akikagua ripoti ya tume aliyounda kuhusu mchanga wa madini. Ikulu/Tanzania
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hii ya pili itakabidhiwa ikulu jijini Dar es Salaam baada ya ile ya awali iliyohusisha wataalamu wa masuala ya miamba na madini kukabidhi ripoti iliyoibua uwepo wa udanganyifu mkubwa kuhusu kiasi cha madini kilichokuwemo katika makontena yanayozuiliwa kwenye bandari za Dar es Salaam.

Kamati ya awali ilibaini kuwa kampuni kubwa za uchimbaji madini nchini humo zimekuwa zikidanganya kuhusu kiasi cha madini yaliyomo kwenye makontena hayo, ambapo ilianisha kuhusu uwepo wa madini mengine mbali na dhahabu hali iliyosababisha kuikosesha Serikali mapato.

Ripoti hii ya pili itakamilisha kazi waliyoagizwa na rais Magufuli ambaye aliunda kamati mbili tofauti huku ya safari hii ikiwa na jukumu la kutathimini athari za kiuchumi na kisheria toka mchanga huo ulipoanza kufarishwa nje ya nchi.

Katika ripoti ya awali rais Magufuli aliagiza kusimamishwa kazi kwa maofisa wa wizara ya nishati na madini akiwemo aliyekuwa waziri wake Profesa Sospeter Muhongo na kuviagiza vyombo vya ulinzi kuwachunguza watu wote waliohusika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.