Pata taarifa kuu
ZAMBIA

Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema akamatwa

Polisi nchini Zambia wamekuwa wakimhoji kiongozi wa chama kikuu cha upinzani UPND Hakainde Hichilema jijini Lusaka.

Kiongozi wa upinzani nchini Zambia  Hakainde Hichildma
Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichildma REUTERS/Rogan Ward
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya mwanasiasa huyo kukamatwa Jumanne asubuhi kwa madai kuwa alizuia msafara wa rais Edgar Lungu mwishoni mwa wiki iliyopita.

Licha ya kukamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi, ripoti zinasema kuwa mamia ya polisi wanaendelea kupiga kambi katika makaazi yake.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter,  kiongozi huyo wa upinzani amedai  kuwa rais Lungu anataka kumuua.

Mwaka uliopita Hichilema alifunguliwa mashitika kwa madai ya kutoa maneno ya  uchochezi.

Hichilema alikabiliana na rais Lungu katika Uchaguzi wa urais mwaka uliopita, zoezi ambalo upinzani umekuwa ukisema kuwa halikuwa huru na haki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.