Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-CHIBOK

Wasichana waliotekwa nyara waachiliwa wakiwa na watoto

Wasichana kumi na nane kati ya 21 walioachiliwa na Boko Haram Alhamisi hii wana watoto, kwa mujibu wa vyombo vya usalama nchini Nigeria.

Baadhi ya wasichana waliotekwa na Boko Haram katika mji wa Chibok, Nigeria.
Baadhi ya wasichana waliotekwa na Boko Haram katika mji wa Chibok, Nigeria. © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Chini ya usimamizi wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu,wasichana 21 waliotekwa nyara mwaka mmoja na nusu uliyopita kaskazini mwa Nigeria wameachiwa baada ya mazungumzo kati ya viongozi wa serikali ya Nigeria na viongozi wa Boko Haram.

Wasichana 21 waliotekwa na kundi la Boko Haram miaka miwili iliyopita, ambao waliachiliwa huru jana, wamekutana na makamu wa rais wa Nigeria Yemi Osinbajo.

Bw Osinbajo amesema wasichana wote wamo buheri wa afya.

Serikali ya Nigeria imekanusha taarifa kuwa wasichana hao waliachiliwa katika kubadilishana na maafisa wa Boko Haram waliokamatwa na vyombo vya usalama vya Nigeria.

viongozi waandamizi wa Boko Haram walikamatwa katika kituo cha polisi cha kukagua magari karibu na mpaka na Cameroon, kwa mujibu wa vyanzo vya usalama.

Suala la kubadilishana wafungwa halikuwepo

"Tafadhali ningependa kuwafahamisha kwamba hapakuwa kubadilishana wafungwa, matokeo ya mazungumzo ya muda mrefu na yenye uaminifu kati ya pande husika," Waziri wa Habari na Utamaduni wa Nigeria, Lai Mohammed, amesem akatika mkutano na waandishi wa habari.

Lakini chanzo cha usalama kimesema kuwa maafisa wa Boko Haram waliachiliwa huru katika kubadilishana na wasichana hao.

Kwa mujibu wa Lai Mohammed, wasichana 197 waliotekwa nyara na wanamgambo wa kundi la Boko Harami hawajulikani walipo.

"Tunaona kuwa hii ni hatua ya kwanza yenye kuamini katika uwezekano wa kuawaachilia wasichana wote wa mjini Chibok wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Boko Haram," Lai Mohammed ameviambia vyombo vya habari.

Wasichana 21 walioachiliwa Alhamisi hii wamepokelewa mjini Abuja na timu ya madaktari na wanasaikolojia.

Serikali yaya Nigeria ina orodha ya mateka walioachiliwa na itawaona familia za wasichana hao kabla ya kutangaza majina yao, kwa mujibu wa Bw Lai.

Mazungumzo yanaendelea, kwa ajili ya kuwaachilia mateka wengine, kwa mujibu wa Garba Shehu, msemaji wa Ofisi ya rais Nigeria.

Jeshi la Nigeria linaendesha operesheni ya usalama kaskazini mwa nchi, hasa katika msitu wa Sambisa, ambao ni ngome kuu ya wapiganaji Boko Haram.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.