Pata taarifa kuu
NIGERIA-MAREKANI

Jeshi la Nigeria latangaza kumjeruhi kiongozi wa Boko Haram

Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa kiongozi wa Boko Haram amejeruhiwa vibaya. Abubakar Shekau inaaminika kuwa amelengwa na mashambulizi ambayo yamesababisha vifo vingi. Jeshi la Nigeria limeleza kuwa mashambulizi hayo ya anga ni ya aina yake.

Askari Nigeria wakati wa operesheni dhidi ya kundi la Boko Haram, Novemba 8, 2015.
Askari Nigeria wakati wa operesheni dhidi ya kundi la Boko Haram, Novemba 8, 2015. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Nigeria limetangaza Jumanne hii Agosti 23 asubuhi, kwa herufi kubwa kwenye akaunti yake ya Twitter: maafisa wengi wa kundi la Boko Haram wameuawa katika mashambulizi ya anga na kiongozi wa kundi la kigaidi, Abubakar Shekau, amejeruhiwa vikali. Maneno yaliyotumiwa yana mashaka kwa sababu jeshi limezungumzia kujeruhiwa mbaya.

Ni vigumu kujua zaidi, kwa sasa, kuhusu ya hali ya afya ya Abubakar Shekau. Msemaji wa jeshi la Nigeria ameiambia RFI saa chache Jumanne hii jioni kuwa Abubakar shekau amejeruhiwa vibaya, huku akibaini kuwa iwapo kutatokea taarifa mpya, atafahamisha.

Jeshi la Nigeria linasema kuwa mashambulizi hayo yalifanyika Ijumaa ya wiki iliyopita wakati wa sala katika kijiji cha jimbo la Borno, karibu na msitu maarufu wa Sambisa unaotumiwa na kundi la Boko Haram kama ngome yao kuu.

Habari hizi zote zinapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari. Ni vigumu kupata uthibitisho kwa sasa, kwa sababu kifo cha Abubakar Shekau tayari kimetangazwa mara kadhaa, na , kwa sababu tangazo la jeshi inaendana sanjari na kuwasili nchini Nigeria kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry.

Jumanne hii Agosti 23, John Kerry amezuru mji wa Sokoto kaskazini mwa Nigeria. Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani amejizuia kutembelea maeneo kunakofanyika mashambulizi ya Boko Haram kwa sababu za kiusalama, lakini mapambano dhidi ya kundi la kigaidi yatazungumziwa katika mkutano wa Kerry na viongozi wa Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.