Pata taarifa kuu
NIGERIA

Kiongozi wa Boko Haram asema bado yupo hai

Kiongozi wa kundi la kigaidi la Boko Haram Kaskazini mwa Nigeria, Abubakar Shekau amesikika akisema kuwa bado yupo licha ya kuwepo kwa ripoti za kiusalama kuwa ameuawa.

Abubakar Shekau kiongozi wa Boko Haram nchini Nigeria
Abubakar Shekau kiongozi wa Boko Haram nchini Nigeria AFP PHOTO / BOKO HARAM
Matangazo ya kibiashara

Shekau amesikika akisema kuwa, watu wanastahili kufahamu kuwa bado wapo na hawawezi kuwafanyia mambo mabaya kwa watu wao.

Katika Sauti hiyo ya dakika 10, Shekau amesikika pia akisema kuwa kundi la Boko Haram litaendelea kutii Koran kitabu kitakatifu cha dini ya Kiislamu.

Mwandishi wa Shirika la Ufaransa la AFP, amesema ametambua sauti hiyo na ni kweli ni ya Shekau ambaye amewahi kutoa sauti kama hizi katika siku zilizopita.

Ripoti zinasema sauti hii imetolewa baada ya kuwepo kwa ripoti kuwa, nafasi ya Shekau imechukuliwa na Sheikh Abu Musab al -Barnawi msemaji wa zamani wa kundi la Islamic State.

Shekau amekuwa akiongoza kundi hili tangu mwaka 2009 baada ya kuuawa kwa Mohammed Yusuf ambaye alikuwa kiongozi wa kwanza wa kundi hilo.

Hadi sasa, kundi hilo limesababisha zaidi ya watu 20,000 kuuawa na wengine zaidi ya Milioni 2 kuyakimbia makwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.