Pata taarifa kuu
MOROCCO-NIGER

Vita dhidi ya Boko Haram: Morocco yaahidi msaada wa kijeshi kwa Niger

Nchi ya Morocco imetangaza kuwa itatoa vifaa kwa serikali ya Niamey ili kukabiliana na mashambulizi ya kila mara ya kundi la Boko Haram kutoka nchi jirani ya Nigeria. Vitakavyotolewa na Rabat ni silaha zisizokuwa za maangamizi na vifaa vinavyoitwa "vya kiusalama.

Askari wa Nigeria wakati wa operesheni dhidi ya Boko Haram, Novemba 8, 2015.
Askari wa Nigeria wakati wa operesheni dhidi ya Boko Haram, Novemba 8, 2015. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Munge mmoja aliyewasiliana na RFI, msaada huu wa kijeshi wa Morocco kwa Niger utaelezewa Jumatano katika Bunge mjini Rabat. Mwaka 2014, Morocco ilisimamia mafunzo ya askari 200 wa Mali katika mbinu za kupambana na ugaidi.

Katika mpango wa kiimani, Morocoo imekua ikipiga vita msimamo mkali wa kidini barani Afrika. Kwa kipindi cha miaka mitatu, Morocco iliwapa mafunzo mamia ya Maimamu kutoka Mali, Guinea na Cote d'Ivoire.

Tangazo la msaada huu wa kijeshi kwa Niger linakuja chini ya wiki mbili baada ya Morocco kurejea rasmi katika Umoja wa Afrika.

Morocco tayari ina mkataba rasmi na 28 za Afrika, lakini mpaka sasa haijapata ridhaa ya Niger. Dhamira ya Morocco katika vita dhidi ya Boko Haram inaweza kuwa hoja ya nguvu ya kushawishi msimamo wa Niamey kwa utawala wa kifalme wa nchi hiyo

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.